Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Simba inatarajia kurejea
mazoezini kujiandaa na
mechi yake ya Ligi Kuu Bara
inayofuatia ambayo itakuwa
ni dhidi ya Mbeya City.

Pamoja na kuanza mazoezi kwenye
Viwanja vya Chuo Kikuu jijini Dar es
Salaam, Simba itatoa zawadi ya mchezaji
bora wa mwezi.
Kawaida Simba imekuwa
ikitoa zawadi kwa mchezaji
bora kila mwezi ambaye
anapatikana kupitia kura
zinazopigwa na mashabiki
wake kupitia mtandao.
Msemaji wa Simba, Haji
Manara amesema mchezaji
bora wa mwezi atalamba Sh
500,000.
"Mchezaji bora wa mwezi
uliopita anatangazwa leo
pale kwenye mazoezi
yatakayofanyika kwenye
Viwanja vya Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam," alisema
Manara.



Chapisha Maoni