Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Licha ya kupanda nafasi nne hadi nambari
136,Tanzania imeorodheshwa ya chini zaidi na
shirikisho la soka duniani FIFA katika soka ya
Afrika mashariki.
Kulingana na orodha ya FIFA iliotolewa siku ya
Alhamisi,Uganda imeorodheshwa ya 75,ikifuatiwa
na Rwanda katika nafasi ya 93.
Uganda na Rwanda zimeshuka nafasi 4 na 15
mtawalia.
Burundi nayo imerodheshwa nambari ya 113
ikiwa ya tatu ikifuatiwa na Kenya katika nafasi ya
131 ikiwa nambari 4.
Taifa Stars ya Tanzania ambayo ililazimu sare ya
0-0 dhidi ya timu ya Super Eagles kutoka Nigeria
katika mechi za kufuzu kwa kombe la Afrika
inashikila nafasi ya 5 na ya mwisho katika Afrika
mashariki ikiwa katika nambari 136 duniani.
Kwengineko orodha hiyo mpya inaonyesha kuwa
Liberia na Afrika Kusini ndizo zilizofanywa vyema.
Mataifa hayo mawili yameorodheshwa ya 95
baada ya kupanda kwa nafasi 65 na 144 baada
ya kupanda kwa nafasi 54 mtawalia.
Kulingana na Shrikisho la FIFA,Ujerumani
inaongoza ikifuatiwa na Argentina kisha Ubelgiji
nafasi ya 3 na Ureno katika nafasi ya nne.



Chapisha Maoni