Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.



Real Madrid pamoja na kuwa nyumbani, imekumbana na kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa wapinzani wake hao wakubwa Barcelona.
Hasira za mashabiki wa Real Madrid sasa zimemuangukia Rais wa klabu hiyo, Florentino Perez na wanataka ajiuzulu kabisaaa.
Uamuzi huo unatokana na wao kuamini hawajibiki ipasavyo na timu hiyo imeingia katika matatizo makubwa ya kushindwa kucheza kwa kiwango huku yeye akiwa kimya.
Mashabiki hao wanaona wamepata aibu kubwa, kwani licha ya kuchapwa mabao hayo manne, lakini Barcelona ndiyo waliotawala mchezo wa dakika zote 90 hiyo jana huku wakionyesha soka la kuvutia kweli kweli.
Mashabiki waliokuwa uwanjani, walikuwa wakizomea huku wakiangalia upande aliokaa Perez ambaye walimuonyesha wanataka aachie ngazi.



Chapisha Maoni