Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


2015 FIFA FIFPro World XI: ROONEY, TERRY NDIO PEKEE WACHEZAJI WA ENGLAND!
Wayne Rooney na John Terry ndio Wachezaji pekee wa England kutajwa kwenye Kikosi Bora cha Dunia cha Mwaka 2015, 2015 FIFA FIFPro World XI, cha Wachezaji 55 kitakachochujwa kufikia Wachezaji 11 hapo Januari 11 wakati wa kutoa Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani, Ballon D'Or.
Kikosi hicho cha Wachezaji 55 kina Wachezaji 10 tu wanaochezea Ligi Kuu England.
Manchester City ndio yenye Wachezaji wengi ambao ni Vincent Kompany, David Silva, Yaya Toure na Sergio Aguero.
Mabingwa Watetezi Chelsea wanao Terry, Branislav Ivanovic na Eden Hazard wakati Manchester United wanae Rooney na David de Gea huku Arsenal ikiwa na Alexis Sanchez.
Real Madrid imetoa Wachezaji 12 kwenye FIFA FIFPro World XI kati ya hao 55, wakati Bayern Munich ina 11 na Mabingwa wa Ulaya Barcelona wana 10.
Uteuzi wa mwisho wa Wachezaji 11 utaamuliwa na Wachezaji wenyewe ambao ni Wanachama wa FIFPro, Chama cha Kutetea Wachezaji Soka wa Kulipwa, kwa kukusanya Kura wa Wachezaji 25,000 toka Nchi tofauti 70.
Kikosi cha FIFA FIFPro World XI kitakuwa na Kipa Mmoja, Mabeki Wanne, Viungo Watatu na Mafowadi Watatu.
FIFA FIFPro World XI-Listi ya Wachezaji 55:
Makipa: Gianluigi Buffon (Italy, Juventus), Iker Casillas (Spain, Porto), David De Gea (Spain, Manchester United), Keylor Navas (Costa Rica, Real Madrid), Manuel Neuer (Germany, Bayern Munich)
Mabeki: David Alaba (Austria, Bayern Munich), Jordi Alba (Spain, Barcelona), Daniel Alves (Brazil, Barcelona), Jerome Boateng (Germany, Bayern Munich), Daniel Carvajal (Spain, Real Madrid), Giorgio Chiellini (Italy, Juventus), David Luiz (Brazil, Paris St Germain), Diego Godin (Uruguay, Atletico Madrid), Mats Hummels (Germany, Borussia Dortmund), Branislav Ivanovic (Serbia, Chelsea), Vincent Kompany (Belgium, Manchester City), Philipp Lahm (Germany, Bayern Munich), Marcelo (Brazil, Real Madrid), Javier Mascherano (Argentina, Barcelona), Pepe (Portugal, Real Madrid), Gerard Pique (Spain, Barcelona), Sergio Ramos (Spain, Real Madrid), Thiago Silva (Brazil, Paris St Germain), John Terry (England, Chelsea), Raphael Varane (France, Real Madrid)
Viungo: Thiago Alcantara (Spain, Bayern Munich), Xabi Alonso (Spain, Bayern Munich), Sergio Busquets (Spain, Barcelona), Eden Hazard (Belgium, Chelsea), Andres Iniesta (Spain, Barcelona), Toni Kroos (Germany, Real Madrid), Luka Modric (Croatia, Real Madrid), Andrea Pirlo (Italy, New York City FC), Paul Pogba (France, Juventus), Ivan Rakitic (Croatia, Barcelona), James Rodriguez (Colombia, Real Madrid), David Silva (Spain, Manchester City), Yaya Toure (Ivory Coast, Manchester City), Marco Verratti (Italy, Paris St Germain), Arturo Vidal (Chile, Bayern Munich)
Mafowadi: Sergio Aguero (Argentina, Manchester City), Gareth Bale (Wales, Real Madrid), Karim Benzema (France, Real Madrid), Douglas Costa (Brazil, Bayern Munich), Zlatan Ibrahimovic (Sweden, Paris St Germain), Robert Lewandowski (Poland, Bayern Munich), Lionel Messi (Argentina, Barcelona), Thomas Muller (Germany, Bayern Munich), Neymar (Brazil, Barcelona), Arjen Robben (Netherlands, Bayern Munich), Cristiano Ronaldo (Portugal, Real Madrid), Wayne Rooney (England, Manchester United), Alexis Sanchez (Chile, Arsenal), Luis Suarez (Uruguay, Barcelona), Carlos Tevez (Argentina, Boca Juniors)



Chapisha Maoni