Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.



Ishu ya beki Juma Nyosso aliyefungiwa miaka miwili kutocheza soka, imeibuliwa upya baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuwa na mchaka mchaka wa kupitia upya na kujiridhi kama hukumu hiyo ni halali a itenguliwe.
Hiyo imekuja baada ya Chama Wacheza Soka Tanzania (Sputa kuwasilisha ombi lao la kufanyika upya kwa zoezi hil takriban wiki moja iliyopita TFF kupitia Bodi ya Ligi ili chini ya Mtendaji Mkuu, Boni Wambura tayari imekubaliana suala hilo.
Katibu Mkuu wa Sputanza, Ab Kasabalala amesema kwamba om hilo waliliwasilisha pamoja ada ya Sh 500,000 kulingana mwongozo uliotolewa huku akisisItiza kuwa hiyo si ruf bali ni kutaka kuona haki ikitendeka kwa mujibu wa tuk lenyewe na adhabu iliyotolew
“Hii adhabu iliyotolewa na kamati ya masaa 72 tunaona haijakaa sawa kwa mchezaji, kipindi alichofungiwa ni kir mno kwa hiyo tumewasilisha kupitia upya tukio na hata vifungu vya adhabu na kuhakikisha haki inatendeka.
“Imeshapokelewa na majibu yametoka kutoka Bodi ya Ligi kuwa muda si mrefu tutakutan pande zote ikiwezekana na mchezaji mwenyewe (Nyosso) a na tuangalie upya,” alisema Kasabalala.
Akiwa anaitumikia Mbeya City, Nyosso alipewa adhabu hiyo baada ya kuingia hatiani kwa kumdhalilisha nahodha wa Azam FC, John Bocco, katika moja ya mechi za Ligi Kuu Bara msimu huu iliyopigwa Uwanja wa Chamazi, Dar na Azam ilishinda 2-1.



Chapisha Maoni