Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Maafisa kadha wa Fifa wamekamatwa kwenye msako wa polisi uliofanywa katika hoteli moja kuu mjini Zurich, Uswizi.
Polisi walifika katika hoteli ya kifahari ya Baur au Lac mjini humo na wakaonekana wakiondoka na watu wawili.
Shirikisho hilo linalosimamia soka duniani limesema litashirikiana kikamilifu na wachunguzi.
Hii ni mara ya pili kwa hoteli hiyo inayotumiwa na maafisa wa Fifa kuvamia na polisi mwaka huu huku tuhuma za ufisadi zikiendelea kulizonga shirikisho hilo.
Mkutano wa siku mbili wa kamati tendaji ya Fifa unaendelea katika mji huo.
“Fifa imefahamu kuhusu hatua zilizochukuliwa leo na idara ya haki ya Marekani,” shirikisho hilo limesema.
“Fifa itaendelea kushirikiana kikamilifu na wachunguzi wa Marekani kama inavyokubalika katika sheria ya Uswizi, pamoja na uchunguzi unaoendeshwa na afisi ya mwanasheria mkuu wa Uswisi.
“Fifa haitasema lolote zaidi kuhusiana na yaliyojiri leo.”



Chapisha Maoni