Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Na Alex Mapunda,Iringa

JUMLA ya wachezaji watano wa  Maji Maji  U-20  walipata nafasi ya kucheza katika mchezo ambao Maji Maji ilifungwa bao   5-1 na Toto Afrika, kufuatia wachezaji wengi wa kikosi cha kwanza kuchelewa kuripoti kambini bila Taarifa.

Uongozi wa timu hiyo wakiwa ligi daraja la kwanza waliwai kuwakata mishahara wachezaji, kwa kosa la kuchelewa kuripoti kambini, hali ambayo inaweza kuwakuta wachezaji wa sasa.

"Kwa wale ambao wamechelewa tumepanga kuwakata mishahara au kuwapa onyo Kali na ikibidi vyote kwa Pamoja,wachezaji ni wafanyakazi kama wafanyakazi wengine naomba kila mmoja afuate sheria na taratibu"
alisema moja ya viongozi wa juu wa timu hiyo.

Kwa upande mwingine mashabiki wa timu hiyo wamesikitishwa na mwendo wa  timu yao na kuhaidi kushirikiana na viongozi lengo kubwa likiwa ni kuinausua timu isije ikakumbwa na mkasi wa kushuka daraja.

Hivi karibuni Maji Maji walikaa kikao na moja  ya makubariano waliyofikia ni kuendesha timu kisayansi pamoja na Mwenyekiti wa chama cha soka Mkoa Golden Sanga kusafiri na timu katika mechi zote za ligi.r



Chapisha Maoni