Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesikitishwa na taarifa zilizosambaa katika mitandao kuanzia jana zikiwahusisha viongozi wa timu moja ya daraja la kwanza na baadhi ya watumishi wa TFF.
Pamoja na kwamba taarifa hizo zilizosambazwa hazihusiani na kesi ya kupanga matokeo iliyoamuliwa siku ya tarehe 03/04/2016, TFF inachunguza kubaini uhalisia (authenticity) wa taarifa hizo na itachukua hatua kali sana kwa watumishi wa shirikisho na viongozi wa timu husika watakaobainika kushiriki vitendo vilivyo kinyume na maadili ya mpira wa miguu.
TFF imekwishaweka bayana nia ya kupambana na yeyote atakayehusika katika upangaji matokeo na uhalifu mwingine unaoharibu ustaarabu wa mpira kwa njia yoyote ile.
Pia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa onyo kwa baadhi ya viongozi, watumishi wa TFF na wadau wa mpira wa miguu kwa ujumla wanaotumia majina ya viongozi wa juu wa TFF katika kufanikisha mipango yao kwa manufaa binafsi.
TFF inawaomba wapenda mpira wa miguu kuwa watulivu na waangalifu wakati  suala hili linashughulikiwa.
Aidha, kuhusu hukumu ya Kamati ya Nidhamu ya TFF ni muhimu ikaeleweka wazi kwamba zipo taratibu za kukata rufaa kwa mujibu wa kanuni ili upande usioridhika na maamuzi yanayotolewa uweze kuhoji maamuzi husika.
Ni vema tukaacha kamati huru zifanye kazi zake kwa mujibu wa taratibu. Kutoa hukumu  mtaani au kwenye vyombo vya habari kunaweza kuwanyima haki wanaostahili na kutengeneza kichaka cha kujificha watenda maovu.



Chapisha Maoni