Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.



Mechi zote kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku
Jumatano Aprili 6
Paris St-Germain v Manchester City
Wolfsburg v Real Madrid

BAADA ya Jana kuchezwa Mechi 2 za kwanza za Robo Fainali ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, Leo pia zipo Mechi 2 za hatua hii huko France na Germany
 Paris St-Germain watacheza na Manchester City wakati huko Germany ni kati ya VfL Wolfsburg na Real Madrid.
PATA TATHMINI FUPI ZA MECHI HIZI:
Manchester City v Paris St-Germain
Hii ni mara ya kwanza kwa Man City kucheza hatua hii ya UCL wakati kwa PSG hii ni mara ya 4 mfululizo kucheza kutua hii.
Timu hizi zimekutana mara 1 tu Ulaya, Desemba 2008, kwenye UEFA CUP Uwanjani Etihad na Mechi kwisha 0-0.
Hii Leo, City wanatarajiwa kuwa nae tena Kipa wao Nambari Wani Joe Hart ambae aliumia Machi 20 walipofungwa na Man United 1-0 kwani sasa yuko fiti.
Akiongea kuhusu Mechi hii, Meneja wa City, Manuel Pellegrini, amesema kila Timu ina nafasi ya kutinga Nusu Fainali na wao hawatacheza Mechi hii ya Ugenini kwa kujihami.
Lakini City itawakosa Yaya Toure na Raheem Sterling ambao ni Majeruhi.
PSG wao wanaweza kumtumia Mchezaji wa zamani wa Man United, Angel Di Maria, ambae alipumzisha Mechi yao ya Jumamosi dhidi ya Nice ya Ligi 1 waliyoshinda 4-1.
Akizungumzia Mechi hii, Kocha wa PSG, Laurent Blanc, aliewahi pia kuichezea Man United, amsema kila Timu ina nafasi ingawa wao wako juu ya City.
Nguzo kubwa ya PSG ni Mshambuliaji wao kutoka Sweden Zlatan Ibrahimovic ambae amepachika Bao katika Mechi zote 4 zilizopita za UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Tegenezi kuu la City ni Sergio Aguero aliefunga Bao 16 katika Mechi 18 alizoanza za UEFA CHAMPIONZ LIGI.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
Paris Saint-Germain: Trapp; Marquinhos, Luiz, Silva, Maxwell; Matuidi, Motta; Di Maria, Cavani, Moura; Ibrahimovic
Manchester City: Caballero; Sagna, Mangala, Otamendi, Clichy; Fernando, Fernandinho; Silva, De Bruyne, Toure; Aguero
REFA: Milorad Mažić (Serbia)

Wolfsburg v Real Madrid
VfL Wolfsburg na Real Madrid hazijawahi kukutana nah ii ni mara ya kwanza kucheza huko Volkswagen Arena Mjini Wolfsburg Nchini Germany.
Wakati Real inatoka kwenye ushindi mkubwa wa kuwachapa Mahasimu wao wakubwa Barcelona 2-1 kwenye La Liga, Wolfsburg wametoka kuchapwa 3-0 na Bayer Leverkusen ikiwa ni Mechi yao ya 3 mfululizo bila ushindi kwenye Bundesliga.
Lakini Meneja wa Real, Zinedine Zidane, amesema wataichukulia Mechi hii kama Fainali.
Zidane amesema: “Hatuwezi kubweteka. Wolfsburg wamepigana kiume na wanastahili kuwa hapa!”

DONDOO MUHIMU:
-Wolfsburg hawajawahi kukutana na Real.
-Real ni moja ya Klabu 2 ambazo hazijafungwa kwenye Mechi za UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu, huu nyingine ikiwa ni Mabingwa Watetezi Barcelona.
-Real hawajafungwa hata Bao 1 katika Mechi zao 7 kati ya 8 za UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu huu.
-Cristiano Ronaldo wa Real ndie aliefunga Bao nyingi kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI kupita Mchezaji yeyote, Bao 90, huku Msimu huu akiongoza akiwa na Bao 13.

Zidane anatarajiwa kukichezesha Kikosi kilekile kilichoifunga Barcelona Jumamosi.
Nae Kocha wa Wolfsburg, Dieter Hecking, amesema motisha kwao si tatizo ingawa hii ni mara ya kwanza kwao kucheza hatua hii ya UCL.
Lakini Wolfsburg itawakosa Majeruhi Sebastian Jung, ambae ni Fulbeki wa Kushoto, na Kiungo Daniel Caligiuri.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
Wolfsburg: Casteels; Trasch, Knoche, Dante, Rodriguez; Guilavogui, Gustavo; Draxler, Schurrle, Arnold; Dost
Real Madrid: Navas; Carvajal, Ramos, Pepe, Marcelo; Kroos, Modric, Casemiro; Ronaldo, Benzema, Bale
REFA: Gianluca Rocchi (Italy)
UEFA CHAMPIONZ LIGI
ROBO FAINALI
Matokeo:
Jumanne Aprili 5
Bayern Munich 1 Benfica 0
Barcelona 2 Atletico Madrid 0      
Ratiba:
Marudiano
Jumanne Aprili 12
Manchester City v Paris St-Germain
Real Madrid v Wolfsburg
Jumatano Aprili 13
Benfica v Bayern Munich
Atletico Madrid v Barcelona
UEFA CHAMPIONZ LIGI
TAREHE MUHIMU:
-Droo ya Nusu Fainali: Aprili 15
Mechi Aprili 26/27 na Marudiano Mei 3/4
FAINALI
Mei 28
San Siro, Milan, Italy


Chapisha Maoni