Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.



 gerrard

Gwiji wa Liverpool, Steven Gerrard amestaafu rasmi kutumikia mchezo wa Soka ikiwa ni baada ya miaka 19 tangu alipocheza mchezo wake wa kwanza wa ushindani mwaka 1998. Gerrard amefanya hivyo akiwa na umri wa miaka 36 kwenye klabu ya LA Galaxy inayoshiriki ligi kuu ya nchini Marekani.
Yapo mambo mengi ya kusimimua kumuhusu kiungo huyo ambaye pia aliwahi kuwa naodha wa Liverpool na timu ya taifa ya Uingereza. Makala hii inakusimulia historia fupi ya kiungo huyu ambaye aliwahi kutamba na Liverpool kabla ya kuelekea Marekani mwaka 2015.
KUZALIWA NA MAISHA YA AWALI KWENYE SOKA
Steven Gerrard alizaliwa tarehe 30/5/1980 kwenye kijiji cha Whiston huko Merseyside. Kijiji hicho kimekatizwa na ile reli maarufu inayounganisha miji mikubwa nchini Uingereza, Liverpool na Manchester.
Gerrard alianza maisha ya soka kwenye timu ya Whiston Junior iliyopo kwenye eneo alilozaliwa kabla ya kujiunga na Liverpool akiwa na umri wa Miaka 9. Gerrard alipokuwa na umri wa miaka 14 alikwenda kufanya majaribio kwenye vilabu mbali mbali bila ya mafanikio. Moja ya klabu ambayo Gerrard alienda kujaribu bahati ni Manchester United.
MECHI YA KWANZA EPL ALICHEZA DAKIKA MOJA
Tarehe 29/11/1998, Gerrard aliichezea Liverpool kwa mara ya kwanza kwenye ligi kuu nchini England. Gerrard alicheza mchezo huo dhidi ya Blackburn  kwa dakika mmoja tu kabla ya mchezo kuisha baada ya kuingia kutokea benchi kuchukua nafasi ya kiungo Jamie Redknapp ambaye alikuwa ameumia.
ANAPATA NAMBA RASMI, ANATWAA VIKOMBE VITATU
Msimu wa ligi 1999/2000 Gerrard alifanikiwa kuwa mchezaji wa kikosi cha kwanza akitengeneza kombinesheni na kiungo Jamie Redknapp kwenye safu ya kiungo ya Liverpool. Msimu wa mwaka 2000/01 Gerrard alitimiza michezo 50 akiwa na Liverpool akifaikiwa kufunga mabao 10
Msimu huo Liverool ilishinda mataji matatu, FA Cup, Kombe la ligi pamoja na ubingwa wa UEFA Cup (sasa inajulikana kama Europa League). Kipindi hicho Liverpool ilikuwa chini ya Kocha Gerrard Houlier
ANAITWA TIMU YA TAIFA KWA MARA YA KWANZA
Mwaka 2000 Gerrard aliitwa kwa mara ya kwanza kwenye timu ya taifa ya England. Aliwakilisha England kwenye mashindano ya Euro 2000, 2004 na 2012.
Pia amecheza mashindano ya Kombe la dunia 2006, 2010 na 2014. Gerrard alitangazwa kuwa naodha wa timu ya taifa ya Uingereza muda mfupi kabla ya kuanza mashindano ya Euro 2012. Hadi anastaafu timu ya taifa Gerrard alifanikiwa kucheza michezo 114 akifunga mabao 21.
ANAPEWA UNAODHA LIVERPOOL
Baada ya kuwa msaidizi wa Sami Hyypia kwenye klabu ya Liverpool, mwaka 2003  Kocha Gerrard Houlier aliamua kumpandisha Gerrard na kuwa naodha mkuu wa Liverpool. Holuier alisema kiungo huyo alikuwa na sifa za uongozi.
SHUJAA WA MAAJABU YA ISTANBUL
Fainali ya ligi ya Mabingwa Ulaya 2004/05 itaendelea kubaki kwenye kumbukumbu za wapenzi wa soka Duniani. Hadi mapumziko kwenye uwanja wa Ataturk Olympic kule jijini Istanbul Liverpool walikuwa nyuma 3-0 dhidi ya Milan.
Kipindi cha pili kilikuwa cha maajabu, Liverpool wakisawazisha mabao yote matatu. Gerrard alifunga bao la kwanza, pia akasababisha bao la tatu baada ya kudondoshwa na kiungo mtukutu Gattuso na kuzaa penalti iliyopigwa na Alonso ambayo iliondolewa na kipa wa Milan Dida lakini Alonso akamalizia tena na kuandika bao.
Gerrard alifunga penalti ya mwisho na Liverpool kuibuka kwa ushindi wa Penalti 3-2.
ASHINDWA KUTWAA TAJI LA EPL
Msimu wa mwaka 2013/14 ulikuwa wa Liverpool, lakini mambo yalibadilika kwenye mechi tatu za mwisho. Liverpool walipoteza mechi moja dhidi ya Chelsea huku Gerrard akifanya makosa yaliyosababisha Demba Ba kufunga bao.
Siku ya mwisho ya Msimu Liverpool ilimaliza katika nafasi ya pili ikiwa na pointi 84 tofauti ya alama mbili dhidi ya Mabingwa  Man City
Gerrard aliondoka rasmi kwenye klabu ya Liverpool mwaka 2015 akiwa amecheza michezo 504 akiwa na mabao 120.

Chapisha Maoni