Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.



Na Alex Mapunda,Iringa
TAREHE 28-03-2024-7:48
TIMU ya soka ya wanachuo wanaochukua mafunzo ya uandishi wa Habari
chuo kikuu cha Iringa zamani kikifahamika kwa jina la Tumaini,wapo
katika mazoezi mazito ili kujianda na mashindano ya Inter-Facuty
yanayotarajia kutimua vumbi hivi karibuni katika dimba la chuo hicho.

Wakizungumza na JELAMBA VIWANJANI baadhi ya wachezaji wa timu ya
waandishi walisema lengo lao kubwa ni kutetea ubingwa wao waliochukua
msimu uliopita ili kuendelea kulinda heshima ya waandishi wa habari
chuo hapo licha ya kupata upinzani mkali toka kwa wanachuo wenzao  wakiwemo BEDA wanaosomea ualimu.

''Sisi tumeanza mazoezi mapema ili kutetea taji letu tumesikia wenzitu
wanachonga sana kuhusu kutunyang'anya ubingwa wasubiri uwanjani sisi
ni vitendo hatuna muda wa kupoteza,Alisema Damas kamara Mlinda mlango
wa waandishi.

"Mpira hauchezwi mdomoni ndio maana sisi tumeanza kufanya mazoezi
mapema ili kuhakikisha kuwa hadi mwisho wa mashindano   tunatangazwa
bingwa kwa mara nyingine,Alisema Michael Msuya.

Timu ya waandishi wa habari imekamiwa sana na wanafunzi wa kozi
zingine kutokana na timu hiyo kuwa na wachezaji wanaojituma katika
mazoezi pamoja na kujitoa kwa moyo kwa ajili ya mpira.

Chapisha Maoni