Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.



Na Alex Mapunda,Iringa

TIMU ya soka ya Lizabon City Pamoja na wapiga pasi wa mchikichini
klabu ya mchikichini Fc zimetinga  hatua ya Fainali katika michuano ya
Gama Cup inayoendelea mjini Songea.

Michuano hiyo ambayo imelindima katika manispaa ya songea kwa mwenzi
mzima sasa yanatarajiwa kuhimishwa tarehe 6 mwenzi wa nne kwa mchezo
wa fainali ambapo tarehe 5 utafanyika mchezo wa kumtafuta mshindi wa
tatu kati ya Songea veterani pamoja na Holly Family watoto wa baba
paroko na joto la pambano hilo limeshaanza kupanda.

Akizungumzia michuano hiyo msimamizi mkuu wa mashindano God Mvula
alisema kuwa timu nyingi katika mashindano hayo zimeonyesha uwezo
mkubwa hali ambayo imepongezwa na mashabiki wa mpira mjini Songea.

Lengo kubwa la kuanzisha michuano hiyo ni kumwenzi doctor Roulance
gama ambaye amefanikiwa kuleta mambo makubwa katika soka la mkoani
Ruvuma kwa kujenga uwanja wa soka wa maji maji pamoja na kuanzisha
timu ya maji maji ambayo ilifanikiwa kufanya vizuri sana miaka ya 1980
hadi mwanzoni mwa miaka ya 2001.

Chapisha Maoni