Mbopa
Luoga
Na Alex Mapunda.
Mbopa
Luoga ni miongoni mwa mabeki imara kuwai kutokea hapa nchini alikuwa moja ya
Beki Hatari ambaye aliumiza vichwa vya washambuliaji hapa nchini miaka ya 1992
hadi 2000 akiwa na Maji Maji ya Songea.
Luoga,Mzaliwa
wa Litui Nyasa, alianza kucheza mpira tangu akiwa shule ya msingi Kibasila
Jijini Dar es Salam ambako Baba yake aliajiriwa katika wizara ya habari na
utamabuni na baadae wakaamia songea Mjini ambapo alibahatika kujiunga na Maji
Maji Kids.Amezungumza na Jelamba Viwanjani na kufafanua mengi:-.
“Nilianza
kucheza Soka la ushindani nikiwa na RTC Songea timu ambayo ilikuwa ikishiriki
ligi daraja la pili ngazi ya Taifa mwaka 1887,sikukaa
sana ndani ya mwaka huo
huo nikatimukia Urafiki ya Dar [timu ya kiwanda cha nguo] hapo nilidumu
kwa kipindi cha miezi 4.
“Lakini
kabla mwaka huo kumalizika tuliitwa na Timu ya Tanesco Songea wachezaji wote
ambao tulienda Urafiki wote tukarudi na kukijenga kikosi cha Tanesco ambacho
kilicheza kwa nidhamu ya hali ya juu na kufanikiwa kupanda ligi kuu toka ligi
daraja la nne nikiwa kama kepteni wa timu.
“Timu
hiyo ya Tanesco ambayo ilikuwa ikiongozwa na kocha Ray Gama[marehemu]
pamoja na Mdachi Kombo ilivyunjwa na Tanesco kwa sababu ambazo hazikutajwa
ingwa ilikuwa imepanda ligi kuu.
“Mwaka
1991 kwa kuwa Tanesco ilivunjwa na uongozi wa timu hiyo ikabadilishwa jina na
ikaitwa Zimanimoto ili kupata nafasi ya kushiriki ligi kuu badala ya Tanesco na
tulifanikiwa kucheza na Yanga,Reli Pamoja na Maji Maji lakini baadae timu
ikasambalatika kwa kuwa tulitakiwa kubaki kazini kama wafanyakazi wa Tanesco.
“Nilitua
Maji Maji mwaka 1992,kipindi hicho nikuwa katika kiwango cha juu sana ambapo
nikikuwa kiboko ya washambuliaji hapa nchini pindi walipokuwa wakikutana na
timu yetu ya Maji Maji, hapo nilicheza kwa muda mrefu Sana na kipindi chote
hicho nilikuwa nikiitwa katika timu ya mkoa wa Ruvuma, ambapo mwaka 2001
nikaachana na soka la ushindani na kubakia kama mchezaji wa Kambalage Veterani
na mfanyakazi wa Tanesco.
Aligoma
kujiunga na Yanga naTukuyu Stars.
“Ndugu
mwandishi mtu yeyote hawezi kuchezea ajira,ni ukweli usiopingika uwezo
wangu wa kusakata kabumbu ulikuwa wa hali ya juu Sana Yanga waliwatuma
wawakilishi wao kuja kunichuka Songea ili kuchezea timu yao kwa kweli sikuwapa
nafasi ya kufanya mazungumzo kwa kuwa nilikuwa naeshimu sana ajira yangu ndani
ya Tanesco.
“Vile
vile Tukuyu Stars waliniitaji ili kukitumikia kikosi chao lakini mimi sikuwa
tayari kujiunga na Timu yeyote Hapa nchini nje ya mkoa wa Ruvuma kwa kuwa
niliogopa kuweka Rehani ajira yangu Toka Tanesco.
Awezi
kusahau
“Nakumbuka
mwaka 1998 mechi kati ya CDA ya Dodoma na Maji Maji ya Songea ambayo
ilichezwa mjini Dodoma kutokana na uimara wa timu yetu tulishinda bao 1-0 ambao
ulichezwa kipindi waeshimiwa wabunge wakiwa Dodoma,bao ambalo lilifungwa na
Maarimu Salehe Romario dakika ya 72.
“Baada ya
Mchezo kuna tukio ambalo alilifanya mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kipindi kile
Mweshimiwa Anna Makinda siwezi kulisahau kwani baada ya kuizamisha CDA
alitukaribishwa kwenye chakula cha mchana.
“Wakati
wa chakula makinda alivua Viatu na akaweka pembeni na akajifunga kanga kiunoni
akawa kama mhudumu, akachukua maji na Kutunawisha mikono wachezaji wote kama
Yesu alivyo waosha miguu mitume wake na baadae akatuletea chakula na
kumpa kila mchezaji, kwa kweli Tukio lile lilitushitua sana kwa
uduma adhimu kama ile pia ilitupa morali ya hali ya juu sana.
“Mimi
sijawai shuudia tukio kama lile naamini ilikuwa mwanzo na mwisho kutokea na
mimi staacha kumwombia makinda kwa mungu kwa wema wake wote ambao aliufanya
akiwa kama mkuu wa mkoa wa Ruvuma kwa Timu Ya Maji Maji.
Ubingwa
wa Maji Maji mwaka 1998.
“Mechi
yetu ya mwisho kombe la Muungano na Prisons ya Mbeya ilikuwa ngumu sana na
tulifanikiwa kupata ushindi kwa mbinde wa bao 2-1 na tukafankiwa kutawazwa
mabingwa.
“Nakumbuka
Yanga tuliwanyang’anya tonge mdomoni kwani walitakiwa wapate ushindi dhidi ya
Kem kem ya Zanzibar ili wachukue ubingwa ambapo walipoteza mchezo kwa kufungwa
bao 2-1 na kutuacha wanalizombe tukichekelea.
“Baada ya
ushindi huo tulipangwa na timu ngumu Toka Misri ya National Alhaly katika
roundi ya kwanza ya club Bingwa Afrika wakatukausha Nyumbani na ugenini ambapo
dar tulifungwa bao 3-0 na Kairo tulichezea kipigo cha bao 2-0 Dakika 5 za
mwisho.
“Kikosi
cha Wanalizombe ambacho kilitwaa ubingwa mbele ya Tanzania prisons katika
uwanja wa sokoine Mbeya wachezaji ambao walicheza alikuwepo Doi Moke,Ali
Mopelo,Omari Husein,Amri Said,Willy Martin,Mbopa Luoga,Dello Ntumba,Twaha
Omari[marehemu],Godfrey Kikumbizi,Said Mshamu Pamoja na David Mjanja. Garrincha
pamoja na Omari Kapilima walikuwepo kwenye Timu ya Taifa.
Walikuwa
wanasali.
“Kipindi
sisi Tunacheza Maji Maji Ushirikina haukuwepo tulikuwa zaidi Tukimtegemea
Mungu na mazoezi ya uhakika ambayo tulikuwa tunayafanya.
“Nakumbuka
Mimi,David Mjanja,Dello Ntumba [mkongomani] pamoja na Daktari wetu wa timu Mzee
Chanangula tulikuwa tukisali pamoja siku moja kabla ya mechi, mara baada ya chakula
cha jioni,mara nyingi ilikuwa kuanzia saa mbili usiku hadi saa Tano.
“Sijui
kama viongozi walikuwa wakifanya mambo mengine kwa Siri lakini mimi walikuwa
wakinifahamu kuwa ni mtu wa sala hivyo hawakuthubutu kuniambia kitu chochote
kinyume na mwenyezi Mungu.
Wachezaji
anaowapenda
“Nawakubali
sana Frenk Domayo wa yanga Pamoja na Messi wa Barcelona wananikosha sana.
Timu ya
Taifa
“Itengenezwe
kuanzia chini ili kuweza kuwa na timu bora, wachezaji waliowengi hapa nchini
hawana uwezo wa kukabiliana na wachezaji wa kutoka nje kwa kuwa uwezo wao ni
mdogo,kuwaendeleza wachezaji wakiwa wamekomaa ni sawa na kumwagilia mmea kwenye
majani.
“Bila
kuwa na Timu za vijana tutachelewa sana kushiriki kombe la dunia,mimi nakumbuka
nilianza kucheza kwenye timu ya Vijana ya maji Maji ali ambayo ilipelekea kuwa
mchezaji mzuri.
Ushauri
kwa Timu Ya Maji Maji.
“Wanaruvuma
wote wawe kitu kimoja na viongozi ili kuiudumia timu kwa moyo mweupe na kama
pesa itukepo katika timu tutakuwa na wachezaji wazuri.
Baada ya
kustaafu
“Hadi leo
bado ni Mfanyakazi wa Tanesco kazi ambayo ni msingi wa maisha yangu pia niliwai
kuwa mwakirishi wa mkutano mkuu TFF toka nikiwa kama mjumbe kisha nikachaguliwa
kama kocha msaidizi katika kikosi cha underseventeen cha mkoa wa Ruvuma ambacho
kilichukua ubingwa wa Tanzania mwaka 2008 na kwa sasa nimetuliwa kuwa katibu wa
kamati ya ufundi na Tiba katika Timu ya Maji Maji Fc.
“Kwa sasa
nina umri wa miaka 49,nina mke na watoto 5,ambapo ni mchezaji wa kambalage
Veterani pia nina timu yangu binafsi ya vijana ambayo inaitwa Matogoro Mabatini
Fc,anaitimisha Mbopa Luoga ambaye wakati akicheza awezi kuwasahau mshambuliaji
wa Jkt Mafinga Bwana Mwalami Pamoja na Sande Manala [Computer] ambao walikuwa
na uwezo mkubwa uwanjani.
mwisho
Chapisha Maoni