ALI YUSUPH SULEIMAN TIGANA, FAHAMU ASILI YA JINA TIGANA.
TIGANA ALIWIKA AKIWA NA SIMBA,YANGA PAMOJA NA TAIFA STARS.
Ilipoishia jana...................
“Mimi nadhani kucheza
kwangu simba ilikuwa tatizo kwa Yanga kwa kuwa kipindi hicho pambano kati yetu
na simba lilikuwa limekaribia, mimi na mwenzangu walitutuumu kuwa tulipokea
pesa Simba ili kufungisha Timu kitu ambacho mimi nilikishangaa sasa na wala
sikuwai fanya ,na kwa bahati mbaya Simba walitufunga Bao 1-0.
Songa nayo………………..
Kutokea kwa ‘Tigana’
“wakati nilipokuwa
Mdogo watu walikuwa wakiniita Ali Kanada kwa kuwa nilikuwa nikivaa Tsherti
ambayo iliandikwa ‘Kanada’ mara kwa mara hasa pindi nilipokuwa nikicheza
mpira katika timu yangu ya Utotoni ya Shauri Moyo Kids,lakini baada yakiwango
changu kukua na kufanya vizuri watu wengi wakaanza kuniita jina la Tigana jina
ambalo nililichukia sana kwa kuwa sikuelewa maana yake.
“na kadili nilivyokuwa
nikilichukia na watu walizidi kuniita baada ya kuona kero nilimfuata mwalimu
wetu wa timu na kumwambia kuhusu jina lile yeye alicheka sana alafu akaniambia
kuwa jina la Tigana lina maana na akaniahidi kuwa tutaangalia mkanda ili kujua
kuhusu jina hilo.
“Basi mwalimu aliniita
pamoja na wezangu akatuwashia mkanda kati ya Blazil na Ufaransa ilikuwa ni mechi
ambayo ilichezwa miaka ya nyuma,ilikuwa ni mechi zuri sana na kocha
akanionyesha kiungo wa ufaransa ambaye alikuwa akifahamika kwa jina la
Jean Tigana kiukweli alikuwa mchezaji mzuri sana mimi awali sikuwai sikia
kuhusu mchezaji huyo ambaye alikuwa mwembamba na sifa kama za mimi.
“Basi kuanzia siku ile
nikawa nafanya mazoezi mara kwa mara na kusikiliza mafunzo ya kocha huku
nikifuata nyayo zake na nilikuwa nikisikia jina hilo nilikuwa nafurahi sana kwa
kuwa walikuwa wakinifananisha na yeye.
Red Stars walinizuia
kucheza msimu mzima.
“mwaka 1992 nyota
nyekundu pamoja na Pan Africa wote waliniwinda ili kunisajili,nyota nyekundu
pamoja na Pan wote walituma watu wao kunitafuta, lakini mimi mwenyewe nilikuwa
na mapenzi na pan na nilikuwa siipendi nyota nyekundu.
“kuna jamaa mmoja wa
nyota nyekundu alikuwa akikaa mtaani kwetu alikuwa akinifuatilia sana
akanichukua mimi na kaka yangu adi ofisini kwa timu yao, mimi nikamwambia kaka
yangu kuwa tuwadanganye mimi nimesaini Timu nyingine hivyo nitashindwa kusaini
kwao,kweli nikawaambi kuwa tayari nilikuwa na mkataba sehemu nyingine hivyo
itaniwia vigumu kusaini kwao.
“ungozi wa Nyota
nyekundu walinipa mkataba na wakaniambia kuwa wapo tayari kurudisha fedha za
timu ambayo mimi nilikuwa nimechukua,kaka yangu baada ya kuona Nyota nyekundu
wanatoa pesa alilainika akanishawishi kusaini mimi sikuwa na mtetezi nikasaini
Mkataba.
“Baada ya kufanya
mazoezi siku nne nikakutana na kiongozi wa Pan nikamweleza kuwa nimesaini Nyota
akanichukua adi ofisini kwao na wakanipa mkataba na wao wakahaidi kurudisha
fedha ambazo nilichukua toka Red Stars,kwa kuwa nilikuwa na mapenzi na Pan
afrika nikasaini mkataba pia nikahama mtaa ambao nilikuwa na nikaa mara ya
kwanza nikaamia mtaa wa Namanga msasani kwa mama mkubwa ili viongozi wa Nyota
Nyekungu wasinione.
“kitu ambacho kilinifanya nisicheze kwa msimu
mzima ni kwamba viongozi wa Pan waliwafuata Nyota na kuwatukana huku
wakiwakebei kuwa hawana pesa hivyo nyota nyekundu wakagoma kupokea pesa toka
Pan na wakasema kuwa wanamtaka mchezaji wao,kwa hali hiyo ilinilazimu kusugua
bechi adi timu ilipopanda ligi kuu hapo nikapata nafsi ya kuanza kuchezea Pan
Afrika katika mechi za mashindano,pia kwa kipindi hicho pia nilikuwa nikichezea
timu ya mtaani hapo ya Namanga Fc.
Timu ya taifa.
“sijisifii ila
kutokana na uwezo wangu mkubwa wa kusakata kandanda nimefanikiwa kutumukia
kikosi cha timu ya taifa kwa misimu mingi sana,ambapo ifuatayo ni baadhi ya
miaka ambayo naikumbuka nimechezea timu ya Taifa,mwaka,1993,1994,1996,1998,2001
pamoja na mwaka 2005 ambao ulikuwa mwaka wangu wa mwisho kuitwa timu ta Taifa.
Itaendelea…………………
Kesho tarehe 27 usikose.
Chapisha Maoni