Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.




Kuchaguliwa kuwa kocha wa manchester united ni moja ya klabu kubwa duniani ,lilikuwa ni jambo la kujivunia kwangu.

Kuchukua nafsi hiyo lilikuwa ni jambo ambalo haliepukiki,sikuwai kujifikiria mara moja mara baada ya kuambiwa kuwa kocha wa united.



Cheo hicho kilikuwa kikubwa sana lakini kamwe sikukata tamaa,hivi ndivyo ilivyokuwa kwa benchi langu la ufundi,nashukuru kwa kujitolea kwa msimu wote.

Tulikuwa tumeelekeza nguvu katika kujenga timu,tuliitaji matokeo mazuri kwa ajili ya mechi za nyumbani na ugenini,lakini ndani ya kipindi hicho cha mpito tumekuwa na matokeo mabaya tofauti na mashabiki wa manchester united walivyozoea,naelewa jinsi walivyoumia.

Ndani ya muda mfupi wa uwepo wangu old trafford na carrington nimejifunza vitu vingi,nawashukuru benchi la ufundi na familia nzima ya united tangu siku ya kwanza,nawashukuru mashabiki walioniunga mkono,nawatakia kila la kheri.

Naamini ukiwa kocha utajifunza siku zote,nitatumia uzoefu wangu nilioupata kujielimisha zaidi ,najivunia kuifikisha  timu robo fainali ya ligi ya mabingwa,namshukuru sir Alex ferguson kwa kuniamini na kunipa nafasi ya kuiongoza united

BY DAVID MOYES.






Chapisha Maoni