Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.



 TAREHE 08-04-2014


 Kivumbi cha michuano ya Kombe la UEFA, kusaka klabu bingwa Ulaya, kinaendelea Jumanne wakati miamba wa England, Chelsea watakapopepetana na miamba wa Ufaransa Paris Saint Germain, PSG katika mchezo wa marudiano hatua ya robo fainali, ambapo Chelsea watakuwa wenyeji.
Chelsea inatarajia kumtumia mshambuliaji wao Samuel Eto'o mwenye umri wa miaka 33 ambaye katika mchezo wa awali ulipigwa mjini Paris, hakucheza kutokana na maumivu ya nyama za paja, lakini Jumatatu alifanya mazoezi.
Mshambuliaji wa pembeni Andre Schurrle, ambaye alitoka nje kutokana na maumivu katika mchezo dhidi ya Stoke Jumamosi huenda akawa imepona na kucheza mchezo wa leo Jumanne.
Chelsea, The Blues wanatarajia kubadilisha matokeo baada ya mchezo wa kwanza kupokea kipigo cha magoli 3-1.
Mchezaji kiungo John Mikel Obi alikosa mchezo dhidi ya Stoke kutokana na kuumia, lakini anaweza kucheza nafasi ya Ramires anayetumikia adhabu ya kadi au kuchukua nafasi ya Nemanja Matic.

Zlatan Ibrahimovic mchezaji wa PSG ya Ufaransa na timu ya taifa ya Sweden

PSG watacheza bila mshambuliaji wao hatari Zlatan Ibrahimovic, ambaye alitoka nje katika mchezo wa awali baada ya kuumia paja katika mechi ya awali katika uwanja wa Parc de Princes.
Raia huyo wa Sweden, ambaye ametikisa nyavu mara 40 katika ligi kuu ya Ufaransa, Ligue 1 msimu huunafasi yake itazibwa na Edinson Cavani.
Mshambuliaji huyo wa Uruguay, ambaye amejiunga na PSG kwa kitita cha pauni milioni £55, msimu wa kiangazi, ni mchezaji tegemeo katika timu ya PSG ya kocha Laurent Blanc anayetumia mfumo wa uchezaji wa 4-2-3-1.
"Cavani' si tu mshambuliaji anayebaki kupokea mipira katika eneo la hatari, bali pia huzuia, hutafuta mipira na huwatisha wapinzani, hilo ni jambo kubwa kwetu," anasema Blanc.
Michezo mingine ya UEFA Jumanne inazikutanisha timu za Borrusia Dortmund ya Ujerumani na Real Madrid ya Hispania. Katika mechi yao ya awali, Borrusia ilichezea kipigo cha magoli 3-0. Mchezo huo ulifanyika mjini Madrid.
Jumatano Manchester United itakuwa inakabiliana na mabingwa watetezi wa kombe la UEFA Bayern Munich ya Ujerumani katika mchezo wa marudiano katika uwanja wa Allianz Arena.
Mchezo wa awali katika uwanja wa Old Trafford, timu hizo zilifungana goli 1-1.
Mchezo mwingine utakuwa kati ya Atletico Madrid na Barcelona. Timu hizo nazo zilitoka sare ya 1-1.





Chelsea FC v Paris Saint-Germain
Chelsea wameruhusu wavu wao kuguswa katika mechi moja tu kati ya tano walizocheza Stamford Bridge dhidi ya timu kutoka Ufaransa lakini PSG wamefunga mabao 14 katika mechi nne za ugenini msimu huu katika mashindano haya na wameshinda mechi zao 6 za mwisho kati ya 11 za UEFA Champions League, wamepoteza mechi 2 tu. 
The Blues wameshinda mechi 7 kati ya 12 za mashindano ya UEFA ambapo mchezo wa kwanza wanakuwa wamefungwa. Waliwatoa SSC Napoli kwa 4-1 baada ya muda wa ziada katika 2011/12 UEFA Champions League raundi ya 16  – walifungwa 3-1 ugenini - walishinda mechi hiyo na kwenda mpaka kutwaa ubingwa. 
   


Borussia Dortmund  v Real Madrid CF
• Ushindi wa Madrid wa 3-0 katika uwanja wa Santiago Bernabéu unamaanisha kwamba wanaweza kuruhusu kufungwa tena 4-1 kama msimu uliopita katika nusu fainali na bado watapita. 
• Madrid wamefunga katika mechi zote za ugenini (22) katika UEFA Champions League tangu walipofungwa 1-0 na Olympique Lyonnais katika hatua ya 16 bora ya msimu wa 2009/10, walitolewa 2-1 on aggregate. Madrid wamefungwa mara nne - mara 3 kati hizo nchini Ujerumani - katika mechi zao 22 za mwisho walizocheza ugenini kwenye mashindano haya.
Over and out: Willian put Chelsea into a 3-0 lead against Stoke with a fantastic curling effort


Chapisha Maoni