Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


TAREHE 08-04-2014Displaying h.JPG

 NI MWENDELEZO WA STORI YA JUMAPILI MWENYEKITI WA MBEYA CITY MUSA MAPUNDA ANAENDELEA KUFAFANUA MENGI KUHUSU MBEYA CITY SONGA NAYO

Unaongereaje  mashabiki wenu  kuleta fujo uwanjani?

“kiukweli jambo hili hata sisi halitupendezi na siyo mashabiki wetu bali ni watu wachache tu wasiyojua maana ya mpira kwa kuwa  mpira ni furaha na burudani na siyo kuleta fujo”

“tutakao wabaini  kuwa ndiyo wanao kuwa chanzo cha kuleta funjo tutawachukulia atua na kuto waruhusu kuingia uwanjani  tukicheza”

Changamoto gani ambazo mnapambana nazo katika ligi

“changamoto kubwa tunayokumbana nayo ni ratiba kwani unakuta ratiba inakuwa ngumu sana  muda wa kupumzika ni kidogo wakati huo timu inatakiwa kusafiri kwenda mbali kucheza,pi changamoto nyingine ni ukosefu wa uwanja wa kufanyia mazoezi suala ambalo  muda mwingine linasababisha tusifanye mazoezi kwa wakati”


Kwanini watu wengi wana ishabikia Mbeya City

“toka timu kabla ya kupanda daraja kulikuwa na ukaribu kati ya viongozi na mashabiki ,ushirikiano na viongozi pia kufanya  vizuri kumewafanya watu wengi waipende timu hiyo”

Gharama za usafiri kwa timu

“ada  na viingilio huwa inatusaidia katika maswala ya usafiri na huwa jezi zikija kila tawi linapewa  kwa mfano katika safari ya kwenda dar juzi timu ilitoa jezi mia kwa kila tawi ambapo faida ndiyo inatusaidia kati shuguli za kuendeshea  tawi letu”


Mnachukuliaje swala la wanasiasa kuwapa sapoti.

“ kama unavyo ona sera yatu sisi ni “Mpira siyo siasa” hivyo hatutawapa nafasi wanasiasa kuingia katika maswala ya mpira wala eti kupitia tawi letu ndiyo afanye njia ya kutuingia kisiasasa sisi tupo kwajili ya mpira tuu”

Tumeona baadhi ya safari mlikuwa mkipewa sapoti na wanasiasa

“nikweli lakini hili siyo sababu ya yeye kutuendesha na ndiyo maana hata kiongozi anapoleta msaada anakutana na sisi viongozi haturuhusu yeye kufanya mkutano na mashabiki wetu”

“hata hivyo vijana sasa tumechoka na siasa tumeamua kuingia katika mpira wanasiasa wamekuwa wakitutumia sana mwisho wasiku tunaishia kupelekwa polisi”

“ukikaa sasa na vijana wa sido na mwanjelwa  wameshaamka maswala ya kutumiwa na wana siasaa hawataki tena kwani kupitia mpira wanapata faida kubwa”

“kunawatu wamesafiri kwenda mikoa mbalimbali kwajili ya mpira  lakini siasa haiwasaidi kitu,tawi letu tuna timu ya sido Fc ambayo kwasasa inashiriki ligi daraja la tatu hivyo tumejikita katika mpira “

kutokana na umahili wa timu hiyo kwa sasa wanampango wa kujenga uwanja ili kujipatika kipato zaidi na kuimalisha timu yao.hivyo timu ambazo zimepanda daraja msimu huu ikiwemo polisi Moro,Ndanda mtwara pamoja  Stendi Fc.


Chapisha Maoni