ALI YUSUPH SULEMAN TIGANA ALIKUWA MCHEZAJI NYOTA HAPA NCHINI.
Ilipoishia jana,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
“Baada ya dili la kucheza mpira Afrika kusini kukwama mnamo 2008
mwishoni nilikwea pipa kuelekea bongo kutokana na kusota nchini Afrika Kusini
kwa muda mrefu bila kupata mkataba licha ya kiwango changu kuwa juu niliamua
kuachana kabisa na soka,anasimulia Ali Yusuph Tigana kisha Anaendelea:-
Itaendelea……………………..
Mvi Bukoba iliambatana na majonzi
ndani ya Simba.
“siku
ya Tukio la kuzama kwa meli ya Mvi Bukoba kila nilikumbuka napatwa na simazi
kubwa sana kwa kuwa tukio lile liliambatana na matukio mengine mawili kwangu,kwanza
siku hiyo simba tulitoka kupoteza mchezo wa kimataifa dhidi ya waarabu katika
Mjini Alexandria nchini Misri,na tukatolewa.
“baada
ya mchezo mishare ya jioni tulipata taarifa kupitia kwa shirika la habari la
kimataifa,CNN kwamba Meli ya Mv Bukoba imezama na watanzania wengi wamepoteza
maisha kiukweli majonzi yaliongezeka mara dufu kwa kuwa tayari tulikuwa na
machungu ya kuaga mashindano hapo tukapeana taarifa huku tukijiandaa kurudi
Tanzania.
“hiyo
ni 9 lakini 10 wakati tuliposhuka uwanja wa ndege jiji Dar es lalam hapo
tulinyong’onyea kabisa kwa kuwa tulipokea Taarifa ya kwamba mchezaji wa Mahili
wa Soka Ramadhani Lemi alikuwa amefariki dunia’anavuta pumzi huku akifuta machozi kutokana na kukumbuka jinsi
ilivyokuwa’kisha anaendelea kusimulia; kiukweli majonzi ambayo tulikuwa
nayo ni makubwa sana basi moja kwa moja tukaenda kwenye mazishi ya mchezaji
mwenzetu,mungu awaweke mahali pema peponi wale wote ambao walipoteza maisha………………………
Endelea
kufuatilia historia ya maisha yake kesho tarehe 22 atasimulia jinsi
alivyokimbia na laki moja ya Dewji.
Chapisha Maoni