Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.




BAADA ya wingu nzito kutanda kwa  David Moyes  kuanzia hapo jana kuhusu kibarua chake hatimaye leo amefukuzwa rasmi yeye pamoja na wasaidizi wake huku ikithibitishwa kwamba Ryan Giggs na Nicky Butt wataiongoza timu hiyo katika michezo minne iliyobakia.


End of the line: David Moyes has been sacked by Manchester United with immediate effect
 David Moyes basi tena Manchester United 

Saying goodbye: United's owners, the Glazer family, lost patience with Moyes after a string of bad results

Klabu hiyo hapo awali ilikuwa imekataa kuzungumzia udaku wa magezti kuwa Moyes atafutwa kazi kabla ya msimu kumalizika.
Moyes, mwenye umri wa miaka 50, aliteuliwa na Ferguson kumrithi alipostaafu mwaka jana baada ya kuwa na klabu hiyo kwa miaka 26.
Taarifa kutoka kwa klabu hiyo imemshukuru Moyes kwa bidii, uaminifu na hekima aliyoonyesha kocha huyo akiwa mkufunzi wa Manchester United.
Moyes alichukuwa usukani wa kuifunza Manchester United mwaka uliopita baada ya aliyekuwa kocha wa siku nyingi Sir. Alex Ferguson kustaafu.
Huku zikiwa zimesalia mechi nne pekee msimu wa ligi kukamilika Mancheseter united inashikilia nafasi ya saba kwenye jedwali la msimamo wa ligi hiyo alama ishirini na tatu nyuma ya viongozi Liverpool.
Klabu hiyo imeshindwa kufuzu kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa ulaya kwa mara ya kwanza katika kipindi cha takriban miaka ishirini.
Hata hivyo mpaka sasa majina ya kocha Uholanzi  Louis Van Gaal, wa Borussia Dortmund Jurgen Klopp, Atletico Madrid’s manager Diego Simeone na Ryan Giggs wanatajwa kuewa nafasi ya kuifundisha timu hiyo kuanzia msimu ujao.


United


Chapisha Maoni