Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


KATIKA kusherekea Sikukuu ya pasaka,Mkoani Ruvuma bondia maarufu wa Ndondi mkoani humo  Musa Omri ameandaa pambano la ngumi la kukata na shoka litakalo wakutanisha  mabondia toka njombe,Kyela pamoja na songea katika uwanja wa michezo wa Maji Maji.

Siku hiyo ya sikukuu ya Pasaka mabondia wataopanda ulingoni ni pamoja na Yunusa Bakari wa Songea atakwaana na  michiel Tyson chinja chinja toka Kyela,Jems Mtanga Songea atapepetana na Mudy Eliya wa Kyela huku mfaume kapungu akizichapa na Sozo boy paulo wa Songea.

Pambano linguine litakuwa baina ya Kasim Mohamed wa songea atapimana ubavu na Omari Omari toka njombe huku wakizindikizwa na mwimbaji wa nyimbo za hasiri Nchunga pamoja God Mgogo ambapo kiingirio ni shiringi elfu tatu kwa wakubwa na elfu mbili kwa watoto.

Akizungumzia pambano hilo mwandaaji musa omari alisema kuwa lengo la kuuandaa
pambano hilo ni kuendeleza mchezo wa ngumi mkoani Ruvuma mchezo ambao unapendwa na watu wengi mkoani humo tatizo ni kwamba wadhamini wengi wanaojitokea  kudhamini mchezo huo sio wa kweli.


Chapisha Maoni