HISTORIA YA KELVIN HAULE AMBAYE ALIWIKA AKIWA NA TUKUYU STARS,MAJI MAJI PAMOJA NA TAIFA STARS.
K HAULE |
ILIPOISHIA JANA………….
“vile vile hapa Tanzania wachezaji wanaibuka tu kutokana na kucheza mitaani na kucheza timu kubwa ambazo zinatuwakilisha katika mashindano ya kimataifa,kwa wenzetu wanakuzwa katika shule za michezo toka wakiwa wadogo,hali ambayo inapelekea timu zetu kufanya vibaya kimataifa.
ENDELEA…………………
Tofauti,FAT-TFF.
kipindi cha Fat wachezaji wa Timu ya taifa Tulikuwa tunacheza katika mazingira magumu sana hasa kwa upande wa vifaa,mara nyingi tulikuwa tunabeba vifaa toka nyumbani ikiwemo viatu na muda mwingine ilitulazimu kufanya mazoezi bila vifaa vyote ali ambayo wachezaji wa sasa ni ngumu kukubariana nayo lakini sisi tuliweza.
“lakini saizi ingawa kuna matatizo kipindi kile yalizidi ila tulikuwa tunafanya vizuri kutokana kwamba wachezaji wa zamani walikuwa wazalendo na walichulia soka kama sehemu ya maisha yao.
Wachezaji ninaowapenda
“nawakubari sana Smomari kapombe,saimon msuva pamoja Salum sure boy ambao ni chipukizi na wapo katika viwango vya juu kwa hivi sasa.
“pia navutiwa na kiwango cha mcheji wa kigeni wa Azam FC toka Ivory Cost kipre Tchetche, ambaye ni moto wa kuotea mbali.
Mafanikio katika Soka
“kiuchumi mpira haujanisaidia sana kwa kuwa kipindi kile hapakuwa na maslai kwa wachezaji zaidi ya kupata pesa ya kula,ila nimefanikiwa kufahamiana na watu mbali mali na kufahamu maeneo mengi katika nchi nyingi.
Ushauri kwa timu ya Maji Maji
“viongozi wa timu ya maji maji wasiongoze timu kwa kutegemea watapata pesa katika Serikali ya mkoa ilo wafute ila wawe wabunifu kwa kutafuta njia mbadala ili kuongoza timu hiyo kwa manufaa ya wanamaji maji.
“wadau wa soka wapo mbali na timu yao ikilinganishwa na zamani,lazima warudishe mawazo yao kwa timu ya Maji maji ili kurudisha maji maji ya ezi zangu ambayo ilitikisa soka la Tanzania.
Maisha baada ya Soka.
“nafanya biashara ndogo ndogo za ujasiliamali ambazo zinaniingizia kipato pia ni Makamu mwenyekiti wa chama cha soka songea mjini [SUFA] pia ni katibu wa chama cha makocha mkoa wa Ruvuma, ingwa sina mafanikio makubwa naishi vizuri na familia yangu.
“ sasa nimeoa na nina watoto watatu wote wa kiume kwangu mimi ni faraja kubwa sana
na naishi nao kwa amani.
Mwisho
ENDELEA KUSOMA JELAMBA VIWANJANI KWA MAKALA NYINGI ZA WANASOKA WALIOWIKA ZAMANI.
Chapisha Maoni