Ali yusuph Suleiman
‘Tigana’alikuwa mchezaji wa kimataifa toka Tanzania kachezea timu nyingi ikiwemo Yanga,Simba,oman,taifa Stars,chelsea ya bongo bila kusahau Malaysia sio makala ya kukosa.
kwa wadau na mashabiki wa soka hapa nchini hasa kwa wale wenye
miaka kuanzia 25 na kuendelea ukipita katika kijiwe chochote na gafla ukasikia
jina la ALI Yusuph Suleiman maarufu kama ‘Tigana’ likitajwa na usimkumbuke!
wakati ni shabiki wa ukweli wa soka,hakika itabidi tukushangae kwa kuwa
tutakuwa na wasi wasi juu ya uwezo wako wa kufikiri,kutokana na uwezo mkubwa
ambao Tigana alikuwa nao pindi alipokuwa akisakata gozi la ng’ombe hapa nchini.
Tigana mzaliwa wa Ilala jijini Dar es salam alianza kusakata kandanda
mwaka 1880 mwaka ambao Tanzania ilipata nafsi ya kushiriki kwa mara ya kwanza
na mwisho michuano ya mataifa ya afrika nchini Nigeria katika shule ya uhuru
changaiko katika mazungumzo na gazeti hili anafafanua mengi kuhusu maisha yake
ya soka:-
“Nilianza kucheza soka la ushindani
katika timu ya Manyema Fc mwaka 1990 timu ambayo ilikuwa ikishiriki ligi daraja
la Tatu katika nafasi ya kiungo mshambuliaji ambapo baada ya kuonyesha uwezo
mkubwa nyota nyekundu na Pan Afrika waliingia kwenye kinyang’anyiro cha
kunisajili ambapo mwaka 1992 nikatua Pan Afrika timu ambayo nilichezea kwa misimu miwili na hatimaye mwaka 1994
nikajiunga na Yanga Africans, kwa kipindi hicho nilikuwa na uwezo mkubwa sana
wa kucheza mpira.
“Umahili wangu na umakini hasa wakati wa kufunga pindi
nikutanapo na timu pinzani uliwafanya simba wanitafute kama chakula pindi mtu
awapo na njaa, toka nilipokuwa Pan na walifanikiwa kuinasa saini yangu mwaka
1996 baada ya kuniwinda kwa kitambo kirefu na nilifanikiwa kuwatumikia wekundu
wa msimbazi hadi mwaka 1998 hapo nilipata nafsi ya kwenda Malayasia.
“Dili la kucheza mpira katika timu ya Malaysia mimi pamoja na mwanamtwa Kiwelo tulifanyiwa na moja ya viongozi ndani
ya simba na tulicheza kule hadi mwaka
2001 hapo nikarudi tena Simba,wakati narudi simba maelewano kati yangu na
viongozi yalikuwa yameyumba kwa kuwa kipindi tupo Maylasia tulizurumiwa sana na
baadhi ya viongizi ambao walitupeleka kule,ambapo dili la kwenda kule pesa zote
walichukua huku tukilipwa mishaara ambayo haikufanana na uwezo wetu wa kusakata
kandanda,kuna kipindi tuligoma kucheza adi walikuja viongozi wa simba
kusuluhisha mgogoro ambapo mimi sikutaka kubaki kule lakini ilitulazimu kubaki
kwa vile hati za kusafiria walikuwa nazo wao ikatulazimu kuendelea kucheza
kinyonge.
“kiukweli Malaysia sisi tulitoa msaada mkubwa sana kwa timu yao
ambapo kabla ya kutusajili sisi timu hiyo ilikaa bila kombe kwa takribani miaka
20 lakini baada ya kutua sisi tukachukua ubingwa wa nchi hiyo,baada ya kurudi
simba uhusiano wangu na viongozi uliyumba kutakana na matatizo ya fedha ya dili
la Malaysia hivyo nikacheza kwa msimu mmoja na baadae nikatimukia yanga na
nikaitumikia timu hiyo toka 2002 adi 2003 apo nikarudi katika timu ya mtaani
kwangu kipindi hicho ilikuwa imepanda ligi kuu nayo nikaitumikia kwa msimu
mmoja na 2004 nikaenda kucheza soka la kulipwa uarabuni katika nchi ya Omani.
“Omani sikukaa sana kwa kuwa nilipewa mkataba wa mwaka mmoja
ambapo ulipoisha mkataba nikarudi Bongo ambapo mwaka 2005 nilijiunga na Timu ya
Moro United maarufu kama chelsea ya bongo kipindi hicho moro walifanikiwa
kushika nafsi ya pili katika ligi kuu ya Tanzania na kuwakirisha Tanzania
katika michuano ya kimataifa.
“nikiwa na moro United tulifanikiwa kucheza vizuri katika mechi
za hawali katika kombe la shirikisho lakini kutokana na wachezaji wachache
wazoefu katika kikosi chetu tulitolewa na timu ngumu ya Et’oe du Sael ya
Tunisia kwa Jumla ya bao 6-1 ambapo kwao walituchabanga bao 4-1 huku nyumbani
wakitushindilia bao 2 mtungi na tukaaga mashindano.
“mwaka 2008 niliamua kutimkia nchini Afrika kusini mara baada ya
timu hiyo kukumbwa na ukata mkubwa ambapo Tajiri aliyekuwa akishikiria timu
hiyo alijitoa kwa sababu ambazo hazikuwekwa wazi na wachezaji wengi nyota
tuliamua kuondoka, nikiwa Nchini Afrika ya kusini nilisota sana kutafuta timu
ya kuchezea kwa kuwa mfumo wa kujiunga na timu za nchini humo ni sawa na Barani
Ulaya ambapo ili timu ikuchukue lazima uende na meneja.
“Mimi nilijaribu bahati yangu katika timu ya Mamelody Sanders
pamoja na Santos lakini niligonga mwamba kwa kuwa sikuenda na Meneja,katika
Timu ya Santos wakati nilipoenda kufanya maojiano na viongozi wa timu hiyo
nilitanguzana na mdogo wangu wakaniuliza huyu ni Meneja? Nikakataa kwa kweli
sikuweza kupata msaada ingawa nilichezea timu hiyo kwa kipindi Fulani.
“Baada ya dili la kucheza mpira Afrika kusini kukwama mnamo 2008
mwishoni nilikwea pipa kuelekea bongo kutokana na kusota nchini Afrika Kusini
kwa muda mrefu bila kupata mkataba licha ya kiwango changu kuwa juu niliamua
kuachana kabisa na soka,anasimulia Ali Yusuph Tigana kisha Anaendelea:-
Itaendelea……………………..
Kesho tarehe 21-4-2014 Atasimulia tukio la kuzama kwa Mv bukoba
pamoja na simba kutolewa katika michuano ya kimataifa siku ya tukio hilo usikose
jelamba viwanjani kila siku.
Chapisha Maoni