David mjanja wapili toka kushoto [waliosimama] |
David Aidani Mjanja ni miongoni
mwa washambuliaji mahili ambao waliwahi tokea na waliwika sana hapa
nchini mnamo miaka ya 1990 -2005,katika club tofauti za ligi kuu hapa nchini,na
Timu ya Taifa.
Mjanja ambaye ni mtoto wa saba katika
familia yenye watoto 8 alizaliwa mwaka 1973 katika Kijiji cha Mdemu mkoani
Dodoma,Ijumaa hii amekutana na Gazeti laChampioni katika maojiano maalum na
kufafanua historia ya maisha yake ya soka kwa kina;
“nilianza kuchieza mpira katika
shule ya msingi mndemu huko Dodoma ,na baada ya kuhitimu elimu ya shule ya
msingi nikajiunga na chuo cha ufundi Makenika N V T C,kwa sasa ni chuo cha
Veta,baada ya kuhitimu nilipata ajira katika kiwanda cha Mazuria Morogoro,hapo
ndipo nyota yangu ilipoanza kunga’aa na nikafanikiwa kupata nafasi ya
kuitumikia timu ya mkoa wa Morogoro
“Ushirika ya Moshi walivutiwa na
uwezo wangu wa kusakata kabumbu nikiwa na timu ya mkoa wa Morogoro ambapo 1991
nikajiunga na timu hiyo hapo nilidumu hadi 1994 ndipo nilipoamua
kutimukia Yanga timu ambayo ilikuwa ikisaka saini yangu kwa udi na uvumba kwa
kipindi kirefu wakati nikiwa na timu ya Ushirika.
Sababu za kuongoka Yanga
“Nilipenda toka moyoni kuchezea
Yanga kwa kipindi Kirefu lakini ilinilazimu kuondoka kwa shingo upandi mara
baada ya kukwaruzana na moja wa kiongozi ambaye alikuwepo katika kamati ya
usajiri kwa sababu ambazo mimi mwenyewe adi leo hii sizifahamu.
“nakumbuka niliambiwa kuwa tayari
jina langu limeshawekwa kwa ajili ya kusainishwa mkataba mwingine,lakini yule
kiongozi akaamua kulikata jina langu na kumweka mchezaji ambaye alikuwa
amemtafuta yeye mwenyewe ili kuniondoa kwa maslai binafsi iliniuma sana na
mwaka 1997 nikaamua kutimukia Maji Maji ya Songea.
“Wakati nikiwa Maji Maji maisha
yalikuwa mazuri kwa kuwa Maji Maji ya kipindi kile ilikuwa na uongozi imara
nikacheza pale hadi 2000 Prisons wakaniona kutokana na uwezo wangu wa kupachika
mabao na wakaamu kunichukua, ambapo nilichezea Prisons hadi 2005 hapo ndipo
nikafikiria kustaafu sokaa.
“Lakini kwa kipindi hicho Prisons
walikuwa na Tawi la Timu yao Tanga ambalo iklifahamika kwa kwa jina la Small
Prisons wakaamua kunipereka Tanga ambako niliendelea kutumikia Timu hiyo.
“Baada ya kuitumikia timu Hiyo kwa
misimu mitatu hapo ndipo nikaona uwezo wangu wa kusakata kabumbu umefikia
kikomo na mwaka 2008,nikatangaza kutundika Daruga,na kuyapa kisogo mambo yote
yahusuyo kandanda.
Hawezi kusahau
“Mwaka 1995,katika meshi ya watani
wa jani Simba na Yanga wakati mimi nipo Yanga kuna tukio lilifanyika Usiku wa
manane katika uwanja wa jangwani unaweza usihamini lakini siku hiyo
alichukuliwa mbuzi mzima na kufukiwa katikati ya uwanja ili kuwaloga Simba.
“Tukio hilo ambalo lilifanyika ndani
ya Dakika kumi na Tano,alichukuliwa mbuzi Mzima huku akiwa amezibwa kwa Pamba
katika maeneo yote ambayo yanatoa Hewa huku kila mchezaji akiwa na mganga wake ,
pakachimbwa shimo huku zikinyunyizwa dawa na kumfukia yule Mbuzi.
“wakati tukiendelea kupewa dawa
zingine wale waganga walitupa masharti na kutuambia kuwa mtu yeyote atakayetoa
siri na kupokea pesa kwa ajili ya kuhujumu timu atakutwa na Adhabu kali Sana.
“Asubuhi tukaamka na tukajiandaa na
mchezo,wakati wa mechi ulipofika tukaingia uwanjani kwa kweli mchezo ulikuwa
mgumu sana kutokana na umahili wa Simba ya kipindi kile Hadi mwamzi wa katikati
alipopuliza kipenga kuhahiria dakika 90 za mchezo zimemalizika Simba 1,Yanga 0
bao ambalo lilipachikwa kimiani na Dua Saidi,siwezi kusahau.
“Nakumbuka wachezaji wa Yanga
walikuwa Steven Nemes,Kenny Mkapa,Salumu Kabunda,Wille Martin,Method
Mogela,Said Mwamba,Mohamed Husein,Edbili Lunyamila,David Mjanja Pamoja na
Sanifu Lazaro,ambayo licha ya maandalizi ambayo timu yetu iliyafanya ndani na
nje ya uwanja tulitoka uwanjani tukiwa vichwa chini.
“Kiukweli ushirikina hauna mchango
wowote katika mpira zaidi ya mazoezi na na kujituma uwanjani, lazima nchi zetu
za kiafrika zibadilike kama tunataka kufika mbali kisoka na pawepo na viongozi
na sio watawala.
.
Haijawai Tokea
“nalikumbuka bao ambalo nililifunga
mwaka 1998 nikiwa na Timu ya Maji Maji ya Songea dhidi ya wekundu wa msimbazi
Simba Toka Jijini Dar Es Salam, mara baada ya Kelvin Haule kuingiza crosi safi
Toka winga ya kulia nami Sikufanya hajizi nikapiga shuti kali golini ambapo
kilichotokea hata mimi sielewi niliupigaje ule mpira Golikipa Joseph Katuba
akiwa amezubaa Pale Golini ule mpira Uligonga mara tatu mwamba wa juu na chini
kwenye chaki mfurulizo…….
Itaendelea endelea
kufuatilia mfurulizo wa makala haya kila siku Jelamba viwanjani
Chapisha Maoni