YANGA SC: TAWI LA TANDALE LILIFUTWA KWA MUJIBU WA KATIBA, TAARIFA
ZINAZOANDIKWA NI UBABAISHAJI TU
TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI
Uongozi wa
Klabu ya Young Africans umeshangazwa na taarifa zilizoandikwa kwenye mojawapo
ya vyombo vya habari juu ya Wanachama wa Tawi la Tandale kusema hawatambui
kufutwa kwa Tawi lao ni za Ubabaishaji.
Mnamo Mei
04, 2014 Mwenyekiti wa Klabu ya Young Africans Bw Yusuf Manji alitangaza
kulifuta Tawi la Tandale kutokana na kua chanzo cha migogoro ndani ya klabu kwa
kipindi cha mrefu, ili hali likiwa halina hadhi ya kuwa Tawi Kamili.
Kufutwa kwa
Tawi la Tandale kunatokana na kutotimiza idadi ya wanachama mia moja (100)
kama inavyojieleza kwenye Katiba ya Yanga SC, Ibara ya 6, kipengele cha 4
“Kutakuwa na uundaji wa matawi katika maeneo mbalimbali hapa nchini na nje ya
nchi. Kiwango cha chini ya idadi ya wanachama ambao wanaweza kunda tawi
kisipungue watu mia moja (100)”.
Ibara ya 13,
kipengele cha 2 kinasema ” Kutolipa ada zake za uanachama kwa muda wa miezi
sita mfululizo bila ya sababu maalum inayokubalika na Kamati ya Utendaji”
Baadhi ya
Wanachama walijifuta uanchama wao kutokana na kushindwa kulipia ada zao za
uanachana kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita, kama inavyojieleza kwenye Katiba
kwamba mwanachama asipolipia ada yake zaidi ya miezi sita moja kwa moja
anajifuta uanachama wake.
Hivyo
Uongozi wa klabu ya Yanga SC unaomba Umma na Wanachama wake Duniani kote
watambue kuwa Tawi la Tandale lilifutwa kutokana na kutokidhi vigezo,
huku wanachama wake wengine watano wakijifuta uanachama kwa kushindwa kulipia
ada zao kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita.
Mwisho
wanachama wa klabu ya Yanga SC wanaombwa kulipia ada zao za uanchama mapema
kabla ya muda wao kumalizika ili waweze kushiriki mkutano mkuu wa marekebisho
ya Katiba utakaofanyika kwenye Ukumbi wa Bwalo la Polisi – Oysterbay Juni Mosi
2014
Beno Njovu
Katibu Mkuu
– Yanga SC
Mei 23, 2014
Chapisha Maoni