Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.




ILIPOISHIA………………


 ''Ajari nyingine ambayo kama si kudra za mwenyezi mungu nilikuwa naondoka duniani ni kukanyagwa na tairi la Basi eneo la Mafinga Iringa,mimi nilikuwa dereva msaidizi kwenye gari letu wakati tupo Mafinga nishuka kwenye gari pembezoni mwa Bara bara kuchukua mzigo gafla nilihisi kitu kinavunja Mguu nikapata nguvu na kuruka kwa kasi kuelekea upande wa pili wa bara bara kumbe gari yetu ilianza kurudi nyuma nikakanyagwa na Tairi ambapo ngozi na nyama toka juu ya ugoko ilikuwa imeshuka chini lakini mara baada ya kufanyiwa vipimo mfupa ulikuwa mzima nikatibiwa na nikaruhusiwa kurudi nyumba,kwa kweli ajari hizi ni rahisi kusimulia ukweli ni kwamba nimeponea chupu chupu.

SONGA NAYO………..

   
Asimulia tukio la
SHAIBU KAMBANGA WAPILI TOKA KULIA KIPA WA ZAMANI WA MAJI MAJI
Sikinde kumtemea mate Mwameja
.  




''Mwaka 1995 wakati wa mechi ya Maji Maji na Simba {Marehemu}  Selestine Sikinde alifanya majaribio mengi sana ya kumfunga Mwameja  ikashindikana kupata bao alichokifanya akamfuata Mohamed mwameja kwa hasira na kumtemea mate usoni, tukio lile limchukiza sana mwameja akaanza kumkimbiza sikinde uwanja mzima mashabiki wote uwanjani wakawa wanashangaa.

  ''Sikinde alitimua mbio moja kwa moja adi kwangu mimi nikamchukua na kumweka mgongoni kwangu  na kumnyoshea mkono Mwameja ishara ya onyo kuwa akisogea angekiona cha mtemakuni kwa kuwa wachezaji wengi walikuwa walikuwa na kukmbukumbu ya tukio nililomfanya mwamzi Shinyanga na katika timu yetu walikuwa wananijua kama kamanda wao Mwameja akasalimu   amri na mwamzi akawapa kadi ya njano kila mmoja,baada ya tukio lile mashabiki walicheka sana na kunishangili kwa kitendo cha kumwokoa Sikinde asichezee kichapo toka kwa mwameja,lakini hadi mwisho wa mchezo matokeo ni 0-0.



Kwanini alifanishwa na Peter Shilton wa Uingereza?.



  ''Mwanzoni hata mimi nilikuwa nashangaa kusikia watu wakiniita kwa jina la Shilton lakini baada ya kuwauliza waliniambia vitu vyangu ninavyovifanya vinafanana na yeye kwa wao mashabiki na wanahabari walikuwa wakiburudika sana pindi niwapo golini.

 ''Kipindi nacheza nilikuwa na uwezo wa kudaka mpira katika mazingira yeyote kutokana na uwezo wangu mkubwa wa kuruka sarakasi hali ambayo ikiperekea kukubaria.

  ''Kwa kipindi kile kila timu ilikuwa na washambuliaji wakatili kiasi kwamba ilikuwa ni ngumu sana kwa magolipa hasa ukizingatia sheria za  kumlinda golikipa zilikuwa nyepesa ikilinganishwa na saizi,pia mimi kwa upande wangu nilikuwa simwogopi mshambuliaji yeyote,mtu ambaye mimi nilikuwa namweshimu kwa kupiga mashuti alikuwa Madaraka Suleiman Mzee wa kiminyio huyo alikuwa balaa lakini kwangu aligonga mwamba adi mwenyewe alijishangaa lakini wakati nipo maji maji yeye nilikuwa namtumia kama mtu wa kunifanyisha mazoezi ya mashuti.

 ''Nakumbuka baada ya mzoezi na mwalimu nilikuwa namwita Madaraka na kunifanyia mazoezi ya mashuti tukiwa pekee yetu,alikuwa anapiga kwenye eneo la penalti na nje ya 18 mara nyingi tulikuwa tunaweka mashuti 40,lakini kutokana na uwezo wangu kati ya mashuti 40 nilikuwa naweza kudaka au kupangua mashuti  35 huku nikiruhusu kuingia kwenye kamba mashuti 4 au 5 pekee hali ambayo ilinifanya niimalike zaidi pindi niwapo uwanja hapo ndipo jina la Shilton lilipotea
.
Itaendelea kesho tarehe 04-05-2014 ambapo atasimulia jinsi ulevi wanawake vinanyochangia kushusha viwanjo vya wachezaji,,,,,,,,,,,,


Chapisha Maoni