Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.



BONDIA MAHILI TOKA MKOANI RUVUMA MUSA OMARI MAARUFU KWA JINA LA KITEPTE.


VIONGOZI wa ngumi za ridhaa mkoani Ruvuma wameshauriwa kusimamia
mchezo huo ipasavyo ili kuendeleza vipaji vya ngumi vilivyopo mkoani
humo.

Akizungumza na championi Ijumaa mchezaji mahili wa ngumi za kuripwa
mkoani Ruvuma musa omari alisema viongozi wa mkoani Ruvuma mara nyingi
wanasahau kutekeleza majukumu yao kwa wachezaji na badala yake
wanajijali wao wenyewe kitu ambacho kinawakatisha tamaa wachezaji.

"viongozi awapo makini kuna kipindi timu ya mkoa ilienda dar
kuwakilisha mkoa, wachezaji walilazwa hoteli ya hali ya chini huku
wakipewa ugari na maharage  lakini viongozi  walilala sehemu nyingine
yenye hadhi suala ambalo liliwakatisha tamaa wachezaji.

''lakini kubwa zaidi  baada ya mashindano wachezaji walilala stendi
kwa tatizo la fedha, mimi niliwatumia nauli ya kurudi songea,alisema Musa Omari.

Omari aliongeza kuwa wachezaji wengi wa ngumi za ridhaa wamekata tamaa
ya kuwakirisha mkoa wa ruvuma kwa kuwa mara nyingi wanakosa uduma za
matibabu pindi wanapoumia wakiwa na timu ya mkoa.




Chapisha Maoni