Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.





Ilipoishia……………………

  ''Sikutaka kwenda kucheza mpira Simba na Yanga bila kazi kwa kuwa viongozi wa timu hizo ni wanafiki sana mara nyingi wanawatelekeza wachezaji katika mazingira ya kutatanisha na wanaondoka mikono mitupu Mfano Omri Husein na John Alex waliachwa na timu hizo na waliathirika sana kisaikorojia.
Songa nayo…………..

 Ulevi ulichangia kupoteza mechi na Mkana Red Devols ya Zambia.

  ''Nakumbuka mwaka 1989  Maji Maji tulitandikwa bao 3-0 katika mechi ya kirafiki dhidi ya Mkana Red Devols toka zambia chanzo kikubwa cha kupoteza mchezo ule wachezaji wa Maji Maji usiku wa kuamkia mchezo walilewa sana kwa sababu walibweteka na sare ya bao 2-2 na  Simba hali ambayo ilipelekea kutoa mwanya kwa wapinzani wetu kucheza kwa nguvu na kutuzidi ujanja.

  ''Nakumbuka siku ile nilicheza vizuri sana kwa upande wetu mwisho wa mchezo wachezaji wa Mkana wakaniita na wakaniambia na cheza vizuri na ili nifike mbali natakiwa kujituma sana katika mazoezi na kumsikiza mwalimu.

 ''Na kingine ambacho kila nikifikiria kuhusu mchezo ule najawa na huzuni,ni kwamba moja ya wachezaji walionipa ushauri toka timu ile wachezaji 6 walipoteza maisha kwa ajali ya ndege  wakiwa na timu ya Taifa ya Zambia hali ambayo inanifanya kujisikia uchungu sana pindi ninapokumbuka tokio lile.


Nimenusurika kifo kwa Ajari mara 3


  ''Ajali ya kwanza ilitokea Misungwi mwanza tulikuwa tunatoka kucheza na pamba ya mwanza dereva  wa basi letu alikuwa amelewa  kwa kuwa toka tulipotoka stendi makonda walisema kuwa hatutafika mbali sisi tukabaki midomo wazi lakini kwa kuwa ilikuwa asubuhi hatukuwa na uhakika kama dereva alikuwa amelewa.

 ''Tukaondoka mwanza huku dereva akiwa mwendo kasi sana na alikuwa kimya muda wote lakini baada ya kusafiri kwa takribani km 40 toka mwanza mjini kuna sehemu bara bara ilikuwa ikifanyiwa matengenezo kwa kuwa dereva alikuwa mwendo kasi gari likamshinda na hatimaye likapinduka.

  ''Mimi niliumia zaidi kuriko wezangu wote nakumbuka nilipasuka sehemu ya kichwa pia nilikatika sikio tukio ambalo liliniweka nje ya uwanja kwa kipindi kirefu na baada ya kupata matibabu ya uhakika nikarejea uwanjani.

  ''Tukio lingine mwaka 2001 muda mfupi mara baada ya kusitaafu soka nikiwa na gari la mkuu wa Wilaya Songea Mjini nilipata ajali Mbaya sana mimi  nikiwa Dereva,nashindwa  kuelezea zaidi kuhusu ajari ile kwa kuwa najisikia uchungu sana kwa mazingara ya ile ajari.

 ''Ninachoweza kusema kuhusu ile  Ajari nilifungwa jela na sikupata msaada toka kwa mtu yeyote wakiwemo Maji Maji ambao niliwatumikia kwa mafanikio makubwa kama sio msamaha wa Rais ningeozea jela.

 ''Ajari nyingine ambayo kama si kudra za mwenyezi mungu nilikuwa naondoka duniani ni kukanyagwa na tairi la Basi eneo la Mafinga Iringa,mimi nilikuwa dereva msaidizi kwenye gari letu wakati tupo Mafinga nilishuka kwenye gari pembezoni mwa Bara bara kuchukua mzigo gafla nilihisi kitu kinavunja Mguu nikapata nguvu na kuruka kwa kasi kuelekea upande wa pili wa bara bara ambapo ngozi na nyama toka juu ya ugoko ilikuwa imeshuka chini lakini mara baada ya kufanyiwa vipimo mfupa ulikuwa mzima nikatibiwa na nikaruhusiwa kurudi nyumba,kwa kweli ajari hizi ni rahisi kusimulia ukweli ni kwamba nimeponea chupu chupu.

Itaendelea kesho tarehe 03-05-2014 ambapo atasimulia tukio la sikinde kumtemea mate mwameja.


Chapisha Maoni