USIKU wa leo dunia itasimama pale watani
wa jadi katika soka la spain watakapovaana kuuania taji la club bingwa barani
ulaya mchezo utakaofanyika saa tatu dakika 45 usiku nchini ureno.
Real Madrid ndiyo klabu yenye
mafanikio zaidi katika Ligi ya Mabingwa, ikiwa imetwaa mataji tisa hadi hivi
sasa.
Hispania kwa ujumla ndiyo inaongoza kutoa mabingwa wengi wa michuano hiyo, hadi sasa ikitoa mabingwa 13, ikifuatiwa na England na Italia ambazo kila moja imetoa mabingwa 12.
Hispania kwa ujumla ndiyo inaongoza kutoa mabingwa wengi wa michuano hiyo, hadi sasa ikitoa mabingwa 13, ikifuatiwa na England na Italia ambazo kila moja imetoa mabingwa 12.
Jumla ya klabu 22 tofauti zimekwishatwaa taji hilo, kati ya hizo 12 zimeshinda Kombe hilo zaidi ya mara moja na tangu michuano hiyo ibadilishwe jina na muundo wake mwaka 1992, hakuna timu iliyoweza kubeba ‘mwali’ mfululizo.
AC Milan ndiyo ilikuwa timu ya mwisho kutetea taji hilo msimu wa 1989–1990 na Bayern Munich, waliokuwa mabingwa watetezi baada ya kuifunga Borussia Dortmund 2-1 katika fainali mwaka jana, walitolewa katika Nusu Fainali na Real Madrid mwaka huu.
Bingwa wa michuano hiyo anatarajiwa kujinyakulia kitita cha Euro Milioni 10.5 na mshindi wa pili Euro Milioni 6.5 wakati timu zilizotolewa katika Nusu Fainali, Beyern na Barcelona kila moja itapata Euro Milioni 4.9.
Je? Nani zaidi kati ya timu hizo
mbili? Tusubiri dakika 90 zitaamua.
Chapisha Maoni