Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.







RAIS wa shirikisho la soka hapa nchini Jamali Malizi anatarajia kuwa mgeni Rasmi katika fainali ya michuano ya Sanga one Cup siku ya jumapili songea mjini ambapo fainali hiyo itapigwa katika uwanja wa Shule ya msingi  ya Bombambili.
Mchuano hiyo ambayo inaandaliwa na mwenyekiti  wa Chama cha soka mkoani Ruvuma [FARU] kila mwaka timu ambazo zimefunzu kucheza fainali ni Tigo Fc pamoja na Bombambili FC ambapo kabla ya mtanange huo timu ya soka ya Holly Family itavaana na walimu manispaa katika mchezo wa fainali.
Akizungumza na championi Ijumaa mwandaaji wa michuano hiyo Gorden Sanga amewapongeza wakazi wa mkoa wa Ruvuma kwa kuitikia kwa moyo mmoja na kufuatilia michuano hiyo adi kufikia hivi sasa pia kwa wale wenye uwezo wa kuandaa mashindano wasisite kufanya hivyo kwa kuwa wachezaji wengi zaidi wataonekana.
“bila mashindano ya mara kwa mara ni kazi bure  katika kuibua vipaji vipya hivyo nawashauri wanaruvuma wenye uwezo kuunga mkono ligi mbali mbali ili vijana wetu wapate muda wa kuonyesha vipaji vyao ambavyo ni ngumu kuonekana kama ligi hazitakuwepo


Chapisha Maoni