Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.




Timu ya soka ya kurugenzi toka mafinga imekamilisha usajili wa wachezaji 25 ili kujiandaa na kipute cha michuano ya ligi daraja la kwanza  mashindano ambayo mkoa wa Iringa unatawakirishwa na timu mbili nyingine ni timu ya lipuli ya Iringa mjini ambapo timu mbali mbali zimeshaanza maandalizi ya michuano hiyo.

Akizungumza na gazeti hili katibu mkuu wa Timu hiyo,Helimark Manga amesema  kati  ya wachizaji hao 25 wachezaji 18 ni wachezaji wapya  huku waliosalia wameongezewa mikataba yao ambapo majina ya wachezaji wote waliosajiliwa yataanikwa  hadharani wekendi hii.

“tunajua ligi itakuwa ngumu sana ndio maana tumeanza kujiandaa mapema lengo ni kupanda ligi kuu ili kukata kiu ya mashabiki wa mafinga na Iringa kwa ujumla kwa kutotazama ligi kuu katika ardhi yao ya nyumbani kwa muda mrefu sasa.

a soka  wa mkoani Iringa waziunge mkono timu zao kwa moyo mmoja ili ziweze kufanya vizuri katika michuano ya ligi daraja la kwanza ambayo itatimua vumbi hapo baadae mwaka huu.


Chapisha Maoni