.
Historia: Ujerumani na Argentina
Mara ya mwisho Argentina kukutana na
Ujerumani katika Fainali 1986.
Argentina na Ujerumani zitachuana
kwa mara ya 3 katika fainali ya kombe la dunia.
Je wajua itakuwa mara ya 8 kwa timu
hizo kuchuana katika kombe la dunia ?
Lakini baada ya Argentina kutinga
fainali ya kombe la dunia huko Brazil dhidi ya Ujerumani Uhasama wa kikanda
baina ya Argentina na Brazil umeibuka upya.
Mashabiki wa Brazil wanaona kheri
kushabiki Ujerumani iliyowaadhibu mabao 7-1 kuliko kuitizama timu wanayoichukia
zaidi Argentina ikitazwa mabingwa wa kombe la dunia mwaka wa 2014 nchini
Brazil,,ni kama msumari kwenye kidonda anasema Sanche raiya wa Brazil,Maoni
yake yanafanana na maelfu kama si mamilioni ya wa Brazil .
Argentina itakuwa inakutana na
Ujerumani kwa mara ya tatu katika fainali ya kombe la dunia ambayo ni rekodi
mpya baina ya mahasimu hao wawili.
Mfungaji mabao mengi ya kombe la
dunia Klose
Aidha Argentina imekutana na
Ujerumani katika mechi zingine 5.
1958
Wajerumani wakiwa ndio mabingwa
watetezi wa kombe la dunia Ujerumani waliibuka washindi mabao win 3-1.
1966
Ujerumani ilitoka sare tasa na
Argentina katika mechi za mkondo wa kwanza .
1986 Fainali
Argentina iliibuka washindi kwa
mabao 3-2 .
Huu ndio mwaka ambao Mshambulizi wa
Argentina Diego Maradona alifunga kwa mkono timu hizo zilipokuwa zimetoshana
nguvu 2-2 hadi katika dakika ya 84 ya kipindi cha pili.
1990 Fainali
UJerumani iliibuka washindi kwa bao
moja kwa nunge kupitia penalti ya dakika ya 85 katika kipindi cha pili.
2006 (Robo fainali)
Messi kuiongoza Argentina dhidi ya
Ujerumani
Huu ndio mwaka ambao Wajerumani
walikuwa wenyeji wa kombe la dunia.
Argentina walikuwa wamewadhibiti wenyeji
wao huko Berlin mechi hiyo ilipokamilika 1-1 katika muda wa ziada .
Die Mannschaft walijifurukuta na
kuilaza Argentina 4-2 kupitia mikwaju ya penalti.(Ujerumani hatimaye ilishindwa
na Italia katika nusu fainali)
2010 (Robo fainali)
Hii ndilo lililokuwa kombe la dunia
la kwanza kuandaliwa katika bara la Afrika na mahasimu hao walikutana katika
hatua ya robo fainali Argentina ikifunzwa na nyota wao Maradona.
Thomas Müller aliiongoza Ujerumani
kuititima Argentina mabao 4-0 .
Mechi hii ndiyo iliyodhibitisha
Thomas Müller na Miroslav Kose ni wa shambulizi wenye haiba ya juu.
Kuanzia wakati huo Argentina
wamekipika kikosi chao upya sasa wakimtumia nyota wao Messi kama mshambulizi wa
pekee.
Hiyo yote ni Historia je Jumapili ni
nani atakayeibuka mshindi ?
Ujerumani ambayo kila mchezaji
anauwezo wa kufunga mabao ama Argentina yenye uwezo mkubwa lakini ikimtegemea
Messi kuifikisha kwenye Fainali ?
BBC NETWORK
Chapisha Maoni