Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.




Michuano ya pool mkoani iringa inatarajia kutimua vumbi mkoani hapa  mwishoni mwa mwenzi wa nane ambapo vilabu vyote vimehaswa kujiandaa vema ili kuhakikisha wanatoa ushindani katika mashindano hayo na kupatikana mshindi wa kweli.

Akizungumza na chanzo cha gazeti hili mkoani hapa mwenyekiti wa pool mkoa salum kisaku alisema wanairinga waendelee kuunga mkono pool na waachane na dhana kuwa mchezo huo ni wa kiuni na badala yake ni mchezo halali na unaweza kumwongezea mtu kipato kwa kuwa mshindi wa michuano hiyo ataondoka na kitita cha kuanzia laki nane pesa ambayo inaweza kumwongezea mtu kipato.
Pia kisaku aliongeza kuwa mchezo wa pool kwa sasa mkoani iringa kama mwitiko utaindelea kuwa mkubwa unaweza kuwa mchezo wa pili baada ya mpira kwa kuwa unachezwa na watu wengi katika maeneo mbali mbali ya mkoa wa iringa.
Aidha kisaku alisema kwa sasa wanajipanga ili kuhakikisha wanaufikisha mchezo huu hadi vijini pia katika wilaya zote za iringa kwa kuwa kwa sasa umeenea zaidi iringa mjini ambako kuna mwamko mkubwa na kuna wachezaji wengi.



Chapisha Maoni