Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.




TIMU ya soka ya lipuli inayoshiriki ligi daraja la kwanza toka mkoani iringa inatarajia kuingia kambini jumapili wiki ijayo katika chuo cha Kilelu eneo la kihasa ili kuanza maandalizi mapema ya kujinoa vilivyo na michuano ya ligi daraja la kwanza inayotarajia kuanza baadae mwaka huu .
Akizungumza na JELAMBA VIWANJANI  katibu msaidizi wa timu hiyo Ronjino malambo alisema ili kuimalisha kikosi hicho tayari wamewasajili wachezaji saba toka nje ya mkoa ambao baadhi yao ni mchezaji wa yanga B Juma chitete,salum keny toka jkt Ruvu pamoja na kipa wa timu ya taifa ya vijana salum pia wamchezaji wenye vipaji wanaopatikana ndani ya iringa wametakiwa kusogea katika kambi hiyo ili kuonyesha vipaji vyao na watapewa nafsi ya kusajiliwa.
“lengo la kuingia kambini mapema tunataka jujipanga vizuri msimu hujao ili kuhakikisha tunapanda daraja wanairinga watambue kuwa timu ya lipuli sio ya viongozi peke yake ni timu ya wanairinga,ili kuipandisha inatakiwa tuwe kitu kimoja ili kuipandisha ilisemama malambo.

Timu ya lipuli toka ilivyoshuka Daraja Takribani miaka 14 iliyopita haijapata tena bahati ya kupanda ligi kuu ambapo mara nyingi imekuwa ikipigana pasipo mafanikio suala ambalo limepelekea  wadau wa soka mkoani hapa kukata tama.




Chapisha Maoni