Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.




TIMU ya Taifa ya Tanzania amepitia maswaibu mengi sana katita vipindi tofauti toka miaka ya nyuma kipidi ambacho wachezaji wengi walikuwa wakijituma sana uwanjani kutokana na mapenzi binafsi toka moyoni na kipindi hicho suala la mishaara kwao ilikuwa ni ngumu kwa wachezaji.
Bila shaka tukizunguzi Taifa stars ya mwaka 1991 hadi 2001 moja kwa moja lazima utamkumbuka Ali  yusuph Suleiman ‘Tigana’ ambaye aliwika akiwa na simba,yanga pamoja na mtibwa sugar ya pale tuliani morogoro katikati ya mashamba ya miwa,ndio!!!!!!!!!
lakini
kwa wadau na mashabiki wa soka hapa nchini hasa kwa wale wenye miaka kuanzia 25 na kuendelea ukipita katika kijiwe chochote na gafla ukasikia jina la ALI Yusuph Suleiman maarufu kama ‘Tigana’ likitajwa na usimkumbuke! wakati ni shabiki wa ukweli  wa soka,hakika itabidi uchunguzwe! kwa kuwa tutakuwa na wasi wasi juu ya uwezo wako wa kufikiri,kutokana na uwezo mkubwa ambao Tigana alikuwa nao pindi alipokuwa akisakata gozi la ng’ombe hapa nchini.

Tigana mzaliwa wa Ilala mpakani mwa mtaa wa Sadani na Newala, jijini Dar es salam alianza kusakata kandanda mwaka 1980 mwaka ambao Tanzania ilipata nafsi ya kushiriki kwa mara ya kwanza na mwisho michuano ya mataifa ya afrika nchini Nigeria katika shule ya msingi uhuru changaiko na nyota yake ikang’aa Zaidi katika timu ya vijana ya shauri moyo kids pamoja na Nambanga Fc bado akiwa mdogo
Pia soka la ushindani alicheza akiwa na manyema fc mwaka 90,nyota nyekundu na pan afrika mw aka 1992,yanga 94,1996 simba1998 malaysia,2000 mtibwa,2001 kurudi simba,2002 yanga,2003 timu ya nyumbani illa fc na baadae akatimukia omani kabla ya kutua chealse ya bongo moro united.

Timu ya taifa.
“sijisifii ila kutokana na uwezo wangu mkubwa wa kusakata kandanda nimefanikiwa kutumukia kikosi cha timu ya taifa kwa misimu mingi sana,ambapo ifuatayo ni baadhi ya miaka ambayo naikumbuka nimechezea timu ya Taifa,mwaka,1993,1994,1996,1998,2001 pamoja na mwaka 2005 ambao ulikuwa mwaka wangu wa mwisho kuitwa timu ta Taifa.
 Hebu sikii hii ambayo ilitokea kwa timu ya taifa ya Tanzania
 Tulisafiri kwa basi na timu ya Taifa adi Zambia.
“mwaka 2003 timu yetu ya Taifa la Tanzania sisi tukiwa wachezaji tulienda kwa usafiri wa Basi toka Dar es Salam adi Zambia isipokuwa wachezaji watatu ndio walienda kwa usafiri wa ndege akiwemo Juma Kaseja pamoja na Pawasa kiukweli tulichoka sana kwa kuwa tulikaa kwenye basi kwa muda mrefu Sana.
“siku ya mechi wachezaji wa timu ya taifa ya Zambia walicheza mpira mzuri sana kushinda sisi kwa kuwa tulikuwa bado na uchovu wa safari ingawa juma kaseja alicheza vizuri sana siku ile hata hivyo zambi walitutungua bao 2-0 na wao wakasonga mbele sisi Tukarudi nyumbi mikono kichwani.
Kweli soka la Tanzania limetoka mbali hadi hivi sasa
Zamani viwanjani ya sports talk itakukumbusha mambo mengi sana kuhusu matukio na mikasa iliyotokea ndani na nje ya Tanzania


Chapisha Maoni