Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.



Robin van Persie ManUtd (cropped).jpg
Kocha wa Uholanzi Lous van Gaal amezua taharuki baada ya kusema kuwa mashambulizi wake matata van Persie anaugua utumbo na kuwa anahofu iwapo atacheza dhidi ya Argentika katika mechi ya pili ya nusu fainali.
Kocha Van Gaal amesema kuwa nafasi yake huenda ikachukuliwa na Nigel de Jong iwapo daktari wa timu hiyo atadhibitisha kuwa van Persie huenda akashindwa kuhimili uchungu na hivyo kukosa mechi hiyo muhimu.
Kwa upande wao Argentina wnaendelea na mazoezi yao kikamilifu ijapokuwa inatarajiwa kuwa Mshambulizi wa Bracelona Lionell Messi atakabidhiwa majukumu  ya kuifikisha Argentina katika fainali yao ya kwanza tangu mwaka wa 1990.
Argentina pia wanatatizika kwa kumkosa mchezaji wa kutegemewa Angel Di Maria ambaye amejeruhi paja lake lakini watakuwa na wasaidizi wake Sergio Aguero na Marcos Rojo ambao watakuwa kwa ajili ya mechi hiyo ya kihistoria kwao.
Uholanzi tofauti na Argentina imefuzu kwa fainali ya kombe la dunia mara mbili zilizopita ikimaliza ya pili mara mbili mfululizo .


Chapisha Maoni