Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Na Alex Mapunda,Iringa
FOMU  za kuuania nafasi mbali mbali za uchaguzi  katika timu ya soka ya lipuli ya  Iringa zimeanza kutolewa ambapo jumla na nafsi saba zimetangazwa kugombaniwa hili kuhakikisha timu hiyo inapata viongozi wazuri ambao wataipandisha toka ligi daraja la kwanza hadi ligi kuu ya Vodacom Tanzania.
 
Akizungumza na JELAMBA mwenyekiti wa uchaguzi wa timu hiyo Jackson Ibrahim Chaula alisema kuwa nafsi za uchaguzi ambazo zimetangazwa na timu hiyo ni nafsi ya mwenyekiti wa timu,makamu mwenyekiti,katibu mkuu pamoja na katibu msaidizi.

Zingine ni mwasibu mkuu,mwasibu msaidizi,pamoja na wajumbe watano ambao watahakikisha timu hiyo inasonga mbele ambapo hawali uchaguzi huo ulitakiwa ufanyike Tarehe 28 mwenzi huu wa nane lakini ikalazimu kusogeza mbele hadi tarehe 28 mwenzi wa tisa kutokana na maandalizi kutokwenda sawa.

“sasa uchaguzi ni mwenzi wa tisa na fomu zimeshaanza kutolewa lakini gharama za fomu ni shiringi elfu 50 kwa nafsi ya mweka azina mkuu,msaidizi pamoja na wajumbe watano lakini nafsi zingine zote zilizosalia ni laki moja, kwa hiyo watu wajitokeze kwa wingi ili kuhakikisha wanapata nafasi ya kuongoza timu hiyo.

Chaula alizitaja sifa za wagombea kuwa ni pamoja na mgombea inatakiwa awe na umri wa miaka 25 na kuendelea,elimu ya kidato cha nne na kuendelea pia asiwe na tuhuma za makosa ya jinai katika kipindi chote cha maisha yake.

Awali uongozi wa lipuli ulilalamikiwa kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo na timu kushindwa kufanya vizuri ambapo kwa sasa watu wanatakiwa kuchukua fomu kilingana na sifa zilizotajwa ili kuhakikisha wanapata nafsi ya kuongoza timu hiyo.


Chapisha Maoni