Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.



Sophia Mwaipyana,Mbeya
Chama cha mpira wilaya ya Mbozi (MBOFA) kimemsimamisha  Charles Mwamlima  aliye kuwa katibu wa kamati ya muda ya chama cha mpira wa miguu wilaya ya  Momba mkoani hapa kwa  kushindwa kutekeleza majukumu kama katibu wa muda.
 Akiongea na JELAMBA katibu  mkuu wa chama cha mpira wilaya ya Mbozi William Mwamlima alisema kuwa kamati  tendaji ya chama kimeamua kumsimamisha  aliye kuwa katibu wa  muda katika wilaya hiyo kutokanana makosa matatu.
“Moja ni kudharau maagizo ya chama cha mpira wilaya ya Mbozi (MBOFA) alishindwa kufwata maelekezo aliyo pewa  kama katibu wa muda “
“Pia kukusanya  pesa katika vilabu kwakuviambia za usajiri nakushindwa kuziwakirisha kwa afisa michezo katika wilaya ya Momba na kushindwa kutekeleza majumkumu yake kama katibu kwani ligi zilikuwa zikiendeshwa ovyo katika wilaya yake”
“Kwakuwa chama cha mpira wa miguu wilaya ya Momba hakikuwa na uongozi  uliyo chaguliwa kwamujibu wa katiba yake chama cha mpila wa miguu wilaya ya Mbozi  chenye mamlaka ya kuendesha  shughuli za michezo  kimeemua kumsimamisha”
“Kutokana na kusimamishwa huko hata ruhusiwa  kujihusisha na shughuli zinazo husu mchezo wa mpira wa miguu na  vitu nyalaka zote zinazo husiana na michezo atavikabidhi kwa  mwenyekiti wa MFA.
Mwisho


Chapisha Maoni