Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Aliyempiga kichwa mwamuzi aadhibiwa


Ismail Gunduz
Mchezaji Ismail Gunduz wa SK Rum ya Austria amefungiwa kuto cheza mechi 70 ikiwa ni adhabu baada ya mchezaji huyo kumpiga kichwa uwanjani mwamuzi wa mchezo.
Gunduz anayechezea timu ya daraja la tano ya SK RUM alimpiga mwamuzi siku ya Jumamosi kwa kichwa muda mfupi kabla ya mwamuzi huyo kupuliza kipyenga cha kumaliza mchezo.
Hata hivyo mwamuzi huyo alikimbizwa hospitali kwa matibabu kutokana na maumivu aliyoyapata baada ya kugongwa kichwa hicho.
Kwa mjibu wa sheria za soka za taifa hilo adhabu ya juu kwa kosa kama hilo ni kufungiwa michezo 108.
BY BBC

WACHEZAJI WAPYA COASTAL UNION KUTAMBULISHWA “COASTAL DAY” SEPTEMBA 7, WAGOSI WA KAYA KUKIPIGA NA POLISI MOROGORO. Kitaifa

???????????????????????????????
NA MWANDISHI WETU, TANGA.

UONGOZI wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga unatarajiwa kufanya utambulisho rasmi kwa wachezaji wote waliosajiliwa kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara unaotazamiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 20 mwaka huu.

Utambulisho huo utafanyika siku ya “Coastal Union day” ambayo hufanyika kila mwaka inapofika Septemba 7 mwaka huu ambao kufanyika mchezo wa mpira wa miguu ambapo msimu huu Coastal Union itacheza na
Polisi Morogoro kwenye uwanja CCM Mkwakwani.

Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema kuwa maandalizi ya kuelekea utambulisho huo yamekamilikwa kwa asilimia kubwa .

Assenga amesema katika kuelekea siku hiyo maalumu kwa timu hiyo wataangalia uwezekano wa kucheza na timu itakayotajwa baadae baada ya mazungumzo kumalizika.
???????????????????????????????
Siku hii itakuwa ni maalumu sana kwa timu yetu tunatarajia tutaweza kufanya jambo hilo kwa wanachama,wapenzi na mashabiki wetu ili waweze kufahamu kikosi chao kabla ya kuanza msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara

Akizungumzia maandalizi ya kuelekea msimu mpya wa ligi kuu,Assenga amesema kuwa maandalizi kwa timu hiyo yanaendelea vizuri kwa wachezaji kufanya mazoezi asubuhi na jioni.
- See more at: http://shaffihdauda.com/?p=5824#sthash.7wwtr15j.dpuf


Chapisha Maoni