Na Alex
Mapunda,Iringa
TIMU ya soka
ya Lipuli imetumia vyema uwanja wake wa nyumbani baada ya kuikung’uta Mlale Jkt
toka songea vijijini bao 1-0 katika mchezo wa ligi Daraja la kwanza uliofanyika
katika uwanja wa samora mkoani hapa.
Mchezo huo
ambao ulikuwa wa kuvutia na kusisimua timu zote zilikuwa zikishambiliana zamu kwa
zamu hali ambayo ilipelekeaa kipindi cha kwanza kumalizika milango ya timu zote
ikiwa imenuna.
Kipindi cha
pili kilianza kwa kasi kubwa huku kila timu ikitafuta bao la kuongoza kwa udi
da uvumba lakini walikuwa ni lipuli ambao walifanikiwa kuwanyanyua mashabiki
wao wachache waliojitokeza uwanjani hapo kwa vifijo na Ndelemo baada ya
mchezaji maili Japheth Vedastus kuwaandikia
Lipuli bao safi Dakika ya 52 kipindi cha pili bao ambalo lilidumu hadi dakika
ya mwisho ya mchezo huo.
Mara baada
ya mchezo huo mashabiki na wadau wa timu ya Lipuli wakiongozwa na Salum kisaku
waliikabidhi Lipuli shiringi Laki moja na Sitini Elfu ili kutoa morali kwa
wachezaji wao ambapo wamehaidi kuiunga mkono timu yao mara kwa mara ili
kuhakikisha inafanya vizuri katika mechi
zake.
Timu ya
Lipuli hadi kufikia hivi sasa imecheza michezo mitano,imetoka sare mara
mbili,ushindi mara mbili na imefungwa mechi moja.
Chapisha Maoni