12 kushiriki
ligi daraja la nne Iringa
Na Alex
Mapunda,Iringa
JUMLA ya
timu 12 zinatarajia kuonyeshana kazi katika michuano ya ligi daraja la nne
Manispaa ya Iringa ambayo yanatarajia kutimua vumbi tarehe 15 mwenzi huu.
Katibu mkuu wa chama cha soka Manispaa ya Iringa
Bakari kamtandi amesema kuwa zaidi ya
timu 12 zilichukua fomu za usajili kwaajili ya michuano hiyo ambapo timu kumi
na mbili pekee zimerudisha fomu na zinatakiwa kufuata masharti yote ya michuano hiyo.
“timu zote
zinatakiwa kulipa ada ya mashindano
ambayo ni shiringi 66,000 na timu ambayo itashindwa kutoa pesa hizo
itakuwa imejitoa katika mashindano,pia kila
timu inatakiwa ijiandae vizuri ili wachezaji waweze kuonyesha uwezo wao
kwa manufaa ya mkoa wa Iringa”alisema
Kamtandi.
Kwa upande
mwingine kamtandi amewataka mashabiki na wadau wa soka mkoani Iringa kuunga
mkono michezo mbali mbali ili kuleta
ushindani hapa nchini ambapo kwa sasa mkoa wa Iringa upo nyuma kimichezo na
mara ya mwisho ligi kuu kuchezwa mkoani Iringa ni miaka 14 iliyopita.
Chapisha Maoni