Na Alex
Mapunda,Iringa
TIMU ya soka
ya Maji Maji Maarufu kwa jina la wanalizombe toka mkoani Ruvuma imezidi
kujikita kileleni baada ya kuendeleza wimbi la ushindi katika mechi zake za
ligi Daraja la kwanza baada ya kuizabua
bila huruma African Lyon toka Jiji Dar es salam.
Mchezo huo
ambao ulifanyika katika uwanja wa maji maji Songea Mjini,African Lyon walikuwa
wa kwanza kupata bao lakini baadae Maji Maji walikuja juu na kujipatia mabao
mawili kupitia kwa Ditram nchimbi Pamoja Maseri Vanventure na kufikisha pointi
15 katika msimamo wa kundi A.
Maji Maji ya
msimu huu inacheza kwa kujituma sana kutoka na mshikamano uliopo ndani ya timu
hiyo ambapo toka imeanza ligi imekuwa ikicheza kwa kujituma sana hali ambapo
imepelekea timu hiyo kuongoza kundi A hadi kufikia hivi sasa wakifuatiwa na
Friends Rangers toka jijini Dar es salam.
Akizungumza
na Championi Ijumaa Meneja wa timu ya Maji Maji God Mvula amesema kuwa kwa sasa
hakuna ubishi moja kwa moja ni kucheza ligi kuu.
“Maji Maji
hoyeee!,mwakani tunacheza ligi kuu pia,tumejipanga kuimalisha zaidi kikosi
chetu wakati wa dirisha dogo licha ya kufanya vizuri,mzunguko huu kikubwa na
kucheza ligi kuu.
Chapisha Maoni