Na Alex
Mapunda,Iringa
Timu ya soka
ya Lipuli toka mkoani Iringa imedhiilisha kuwa mwaka huu imepania kupanda
daraja baada ya hapo juzi kuifumua kimondo Fc Toka Mbozi mbeya bao 1-0 Katika
mchezo mkali na wakuvutia wa ligi Daraja la kwanza uliopigwa katika uwanja wa
samora mkoani hapa.
Katika
mchezo huo timu ya Lipuli ilijipatia bao pekee kipindi cha pili kupitia kwa mchezaji machachari Amburos Mbilo mnamo
dakika ya 74 ya mchezo na kupanda hadi nafsi ya tatu katika msimamo wa kundi A
ambapo kundi hilo linaongozwa na Maji Mji ya Songea,wakifuatiwa na Friendi
Rangers zote zikiwa zimejikusajia pointi 12 baada ya kucheza mechi 6,huku Lipuli
ikiwa na pointi 10.
Akizungumza
na JELAMBA VIWANJANI Katibu Msaidizi wa Timu ya Lipuli Ronjino Malambo alisema
Jumatano hii hapo watavaana na timu ya Villa Squad toka jijini Dar es salam timu
ambayo inashika nafsi ya 11 huku ndugu zao African Lyon wakiburuza mkia katika
kundi hilo.
Kwa pande
mwingine timu ya soka ya Kurugezi
ilitoshana nguvu na Maji Maji sc wanalizombe toka Songea katika uwanja wao wa nyumbani ambapo hadi
kufikia hivi sasa wanakamata nafsi ya 6 wakiwa na pointi 8 kibindoni baada ya
kucheza michezo sita.
Ligi ya Mkoa
Iringa sasa ni novemba 15
Chapisha Maoni