Steven
Fletcher amefunga mabao mawili na kuisaidia timu yake ya Sunderland
kuinyuka Crystal Palace 3-1 kwenye dimba la Selhurst Park na kujitoa
kwenye shimo la kushukia daraja la ligi kuu ya England.
Katika
mchezo huo pekee wa jumatatu usiku Fletcher aliifungia timu yake bao la
kuongoza kabla ya mlinzi wake Wes Brown hajaisawazishia Palace kwa bao
la kujifunga mwenyewe. Sunderland waliongeza mapigo pale Jordi Gomez
alipoutia wavuni mpira kwa kombora la chini kabla ya Mile Jedinak
hajatolewa nje kwa kadi nyekundu kufuatia kuonyeshwa kadi ya njano ya
pili kutokana na mchezo mbaya. Ushindi huo umemaliza mwendo mbovu wa
Sunderland katika ligi hiyo baada ya hivi karibuni kuambulia vichapo
mfululizo na sasa wamepanda hadi nafasi ya 15 na kuziacha shimoni
Leicester City, QPR na Burnley…
Asante kwa kutembelea Hope FM Iringa, Asante kwaku-share habari hii, Kama una Maoni, Ushauri, Story ya ku-share na sisi na au Unahitaji msaada...!
Wasiliana nasi kwa Email hopefmiringa@gmail.com au ungana nasi kupitia mitandao ya kijamii hapo chini!
Wasiliana nasi kwa Email hopefmiringa@gmail.com au ungana nasi kupitia mitandao ya kijamii hapo chini!
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni