Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


X

Standings


NAFSI
TIMUMPWDLGFGA+/-Pts

1
Mtibwa Sugar642092714

2
Coastal Union632185311

3
Azam631263310

4
Young Africans631275210

5
Kagera Sugar62315329

6
Mgambo JKT630345-19

7
JKT Ruvu621357-27

8
Ruvu Shooting621346-27

9
Simba SC60606606

9
Tanzania Prisons61326606

11
Ndanda6204810-26

12
Polisi Morogoro613257-26

13
Stand United613249-56

14
Mbeya City612325-35


Ligi kuu soka Tanzania Bara jana iliendelea kwa mechi moja ambapo timu ya Mgambo JKT ilishuka kwenye dimba la Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga kuchuana na Mbeya City.
Awali mechi hii ilikuwa ichezwe siku ya jumapili lakini hilo halikuwezekana kutokana na mvua kusababisha dimba la Mkwakwani kujaa maji.
Katika mchezo huo Mgambo JKT iliibuka na ushindi wa mabao 2 – 1 dhidi ya Mbeya City. 
Malimi Busungu aliipatia Mgambo la kwanza dakika ya kumi ya pambano kwa mkwaju wa penati mara baada ya Fully Zully Maganga kuangushwa ndani ya eneo la hatari na mwamuzi Israel Nkongo kuashiria penati ipigwe.
Iliwachukua Mgambo JKT dakika kumi na tatu kuongeza bao la pili na la ushindi kupitia kwa mshambuliaji Ally Nassoro Iddy.
Bao la kufutia machozi la Mbeya City lilifungwa dakika ya 76 mnamo kipindi cha pili. Deus Kaseke alitumia vizuri pasi ya Stephen Mazanda na kumtungua mlinda mlango, Salehe Lubawa kwa shuti la mbali.
Ushindi huo umeipandisha Mgambo JKT hadi nafasi ya sita baada ya kujikusanyia pointi tisa. Kwa upande wa Mbeya City, hicho kinakuwa kipigo cha tatu mfululizo kwenye Ligi Kuu huku wakiendelea kuvuta mkia kwa pointi zao tano.
X




Chapisha Maoni