Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


 
KOCHA mkuu wa yanga marcio Maximo anatarajia kutua hapa nchini   kesho akiwa  na kifaa kipya toka Brazil Emerson Oliveira Neves Roque  ili kuziba nafsi ya Jaja ambaye inaelezwa kutupiwa vilago.

lakini kufuatia kuondoka kwa Jaja baadhi ya viongozi wamepokea taarifa hiyo kwa masikitiko makubwa huku wengine wakisema kuwa hana bahati na yanga.

“Siamini kama Jaja kaondoka kweli, lakini mpira ndivyo ulivyo ingawa alionekana kutokukubalika kwa baadhi ya mashabiki, lakini upande wangu nilikuwa namkubali na kuna baadhi ya mechi aliisaidia timu,” alisema Dida.

“Yanga ni timu kubwa na wachezaji wake wote wana uwezo siyo kweli kwamba bila Jaja timu haiendi hivyo huenda riziki yake Yanga ndiyo imeishia hapo atatokea mwingine ambaye ataziba pengo lake kwani naamini Yanga ina washambuliaji wengi,” alisema Dida.
pia Tegete alisema:”Sijui kama Jaja kaachwa ndiyo unaniambia wewe. Daah kama kweli basi haikuwa riziki yake kukaa Yanga muda mrefu japo ni mchezaji mzuri.

Jaja alifanya vizuri katika mechi za kirafiki lakini baada ya ligi kuanza alionekana kumbwela ambapo marcio ameamua kumreta Mbrazil mwingine kufanya majaribio ili kuziba pengo lake.


Chapisha Maoni