Na Alex mapunda,Iringa
Mwili wa ailiyekuwa mwasisi na
mlezi wa timu ya Lipuli ya Iringa Jumanne Mwalwango, umezikwa kwa heshima zote
katika makaburi ya Mlolo Iringa manispaa.
Mwalwango ambaye allifariki dunia
hivi karibuni akiwa na umri wa miaka 75,alikuwa na mchango mkubwa ndani ya
Lipuli toka kipindi hicho ikifahamika kwa jina la Tahita na amekutwa na umahuti
katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa kwa ugonjwa wa moyo.
Akizungumza na Jelamba Katibu
msaidizi wa Timu hiyo bwana Ronjino Malambo alisema kuwa kumpoteza mzee
Mwalwango ni pengo kubwa ndani ya timu kwa kuwa yeye alikuwa kama dira ndani ya
timu hiyo na alikuwa kipaombele katika kutoa maamzi yenye tija ndani ya Lipuli.
“safari hii tumeondokewa na mtu
muhimu sana ndani ya Lipuli,tungeweza kumrudisha tungefanya hivyo lakini
hatuwezi kwa kuwa ni mapenzi ya mungu,mzee wetu alikuwa mshauri,mlezi pia muda
mwingine alisimama kama kiongozi na baba wa timu, pengo lake ni kubwa
sana”Alisema malambo huku akitokwa na machozi.
Lipuli ilianzishwa mwaka 1972 na
mzee Jumanne mwalwango toka alipokuwa kijana akaanza kuitumika timu ya
Lipuli,mungu amlaze mahali pema peponi ameni!.
Chapisha Maoni