Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.



Na Alex Mapunda,Iringa
TIMU ya maji maji imeendelea kuwadhiilishia wadau na wapenzi wa timu hiyo kuwa imepania kupanda ligi kuu Msimu huu baada ya kuanza mzunguko wa pili kwa kuifumua Ashati United wauza mitumba wa Ilala bao 1-0 ugenini.

Maji Maji mabingwa wa kombe la muungano mwaka 1985,1986 pamoja 1998 hadi kufikia hivi sasa wamefikisha pointi 27,ambao wanafuatiwa na Lipuli ya Iringa pamoja na Afrikan Sports ya Tanga ambao wote wanapointi 23 katika msimo wa kundi A.

Meneja wa Maji Maji God Mvula amekiambia chanzo cha Gazeti hili kuwa siri ya maji maji ya kufanya vizuri hadi hivi sasa ni mshikamano  uliopo baina wachezaji,viongozi,mashabiki pamoja na wadhamini wa timu hiyo ambao wamejitoa kwa asilimia kubwa ili kuhakikisha timu inasonga mbele.

“Maji maji ligi kuu hiyo aina ubishi,tunacheza ili kukamilisha ratiba,tumesota muda mrefu bila kupanda sasa wakati wetu umefika”alisema Mvula.

Pia mvula amewapongeza waamuzi kwa kuchezesha vizuri katika mechi mbali mbali ambazo maji maji wamecheza ambapo kuwataka kuendelea kufuata sheria 17 za kandanda ili kudumisha taaluma yao.

Maji maji wanatarajia kushuka uwanjani Tarehe moja siku ya Alhamisi kuvaana na Tessema Fc katika uwanja wa mkwakwani Tanga.


Chapisha Maoni