Afisa mkuu wa maadili anayehusika na
uchunguzaji katika wa shirikisho la soka duniani FIFA ,Micheal Garcia
amejiuzulu.
Bwana Garcia aliongoza uchunguzi wa
FIFA kuhusu vile kandarasi za kombe la dunia la mwaka 2018 na 2022
yalivyotolewa kufuatia madai ya ufisadi.
Katika taarifa yake ya kujiuzulu
Bwana Garcia amesema kuwa kuna ukosefu wa uongozi katika FIFA na kwamba alikuwa
amepoteza imani na mwanachama mwenzake katika kamati hiyo jaji mjerumani
,Joachim Eckert ambaye alisema hakusema ukweli kuhusu matokeo ya uchunguzi
wake.
Wanachama wa kamati hiyo ya maadili
wameamua kutochapisha matokeo ya uchunguzi wa bwana Garcia.
Chapisha Maoni