AZAM FC leo jumapili inavaana na El Merreikh ya Sudan mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa na morali ya ajabu kutokana na maandalizi ambayo timu hiyo imeyafanya ambapo mchezo huo utafanyika katika uwanja wa chamazi .
Azam iliyoanzishwa mwaka 2007 na inayoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika mara ya kwanza, itaivaa El Merreikh, timu kongwe katika mashindano hayo baada ya kushiriki mara 19, lakini haijawahi kuchukua ubingwa hata mara moja.
Kocha mkuu wa Azam, Mcameroon Joseph Omog, amesema anaijua vizuri El Merreikh yenye wachezaji wajanja kama, Mkenya Allan Wanga na Mmali Mohamed Traore, lakini haimpi presha na alichopanga ni kuwachapa mabao mengi.
“Naijua Merreikh, si wageni kwangu hata kidogo ni wajanja sana, wana wachezaji wazuri kama Traore na wazoefu lakini nimejiandaa kwa yote,” alisema Omog na kuficha silaha na mbinu wanazotumia wapinzani wake.
Timu zote
mbili ni tajiri na zimepania kufanya makubwa ili kufika mbali kisoka tofauti na
zilivyo Simba na yanga hapa nchini tusubiri tuone soka safi leo chamazi Mungu
ibariki Azam,mungu Ibariki Tanzania.
|
|||||||||||||||||||||||||||||
Chapisha Maoni