Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.





Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania (TFF), limezitakia kila la kheri na ushindi timu za Azam na Young Africans katika michezo yao ya marudiano ya michuano ya vilabu barani Africa itakayofanyika mwishoni mwa wiki hii . TFF, kupitia Afisa Mawasiliano wake, Baraka Kizuguto imesema ina amini timu hizo zitapeperusha vema bendera ya nchi.
Azam FC itakuwa ugenini siku ya Jumamosi mjini Khartoum, Sudan kucheza mchezo wa marudiano na wenyeji timu ya El Merreikh katika kombe la Washindi barani Africa (CAF Champions League) ambapo katika mchezo wa awali uliofanyika Chamazi jijini Dar es salaam Azam iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Jijini Gaborone nchini Botswana katika kombe la Shirikisho (CAF Confederation Cup), timu ya Young Africans watacheza na wenyeji timu ya jeshi ya BDF XI siku ya ijumaa katika mchezo wa marudiano pia, ambapo katika mechi ya awali Young Africans iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Mjini Zanzibar KMKM wataikaribisha timu ya AL Hilal ya Sudan siku ya Jumamosi katika Uwanja wa Aman, huku kikosi hicho Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM) kikihitaji ushindi wa kuanzia mabao 3-0 ili kuweza kusonga mbele, kufuatia kupoteza mchezo wa kwanza Khartoum kwa mabao 2-0.
Timu ya Polisi Zanzibar itakuwa mwenyeji wa timu ya FC Mounana kutoka nchini Gabon siku ya jumapili katika mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika,ikihitaji ushindi wa mabao 5-0 ili kufuzu hatua inayofuata baada ya kupoteza mchezo wa awali kwa mabao 4-0.


Chapisha Maoni